Saturday, February 27, 2010

SWALI LA KIZUSHI???????

leo nilikuwa natengeneza mkanda wa saa pale mtaa wa Maktaba ( kati kati ya jiji la Dar Es Salaam), baada ya matengenezo nikadaiwa 'Buku Jelo'

Nikatoa macho na kushangaa, wadau nilikuwa nadaiwa bei gani?

Thursday, February 25, 2010

MBONA HATUTUMII RASLIMALI ZETU?

Dola nyingi za kiafrika zinawaangalia wapiga kura wake kwa jicho la dharau, kutowajali na kufanya kazi kwa mazoea bila kujua kuwa wao ndiyo 'engine' ya maendeleo. Matokeo yake dola hizi zinashawishika mara kwa mara kukimbilia nchi za nje kuomba misaada.

Siye wananchi kwa makundi yetu twaweza, wala hatuhitaji $$$ kuendesha maisha yetu.Tunapozongwa na matatizo mengi twatafuta njia mbadala ya kutatua matatizo yetu na twaiweka kando serikali kuu, twazipiga kisogo serikali za mitaa, na kujihimu wenyewe.

Sasa hii ina maana gani? wakati dola inapokosa kuwajibika kwa wapiga kura wake, kinachotokea ni kwamba wapiga kura nao hawaoni umuhimu wa kuwajibika kwa dola. Wengi hatulipi kodi, na wala hatuoni umuhimu wa kufanya hivyo. Lakini kodi tunayolipa ni kwa njia tofauti na labda hatuoni kuwa ni kodi halali. Tunapotoa michango ya harusi hiyo ni kodi ya aina yake kwani tunategemea huyo tunayemchangia naye atusaidie wakati wa shida; tunapotembelea wagonjwa hospitali tunawekeza kwa ajili ya matatizo ya usoni; tunapohudhuria misiba hatupotezi muda ila ni amana tunayorudishiwa pale na siye majanga yatakapotugusa. Waingereza wanasema, 'scratch my back and I will scratch yours'.

Wala hatuhitaji kwenda nchi za magharibi kuomba misaada!!!!! Baba wa Taifa aliwahi kusema hivi, ' Ili tuendelee twahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watu tunao wengi tu na kwa kweli uwiano wa wanaozaliwa huku juu kuliko wanaokufa; ardhi tunayakutosha, ila kinachokosekana ni siasa safi na uongozi bora wa kutumia vizuri raslimali watu na ardhi nchi iliyojawaliwa na Mwenyezi Mungu. Majuzi tulishuhudia janga la mafuriko kule kilosa, Morogoro. Nguvu tulizonazo kama watanzania zilijidhihirisha pale ambapo Radio binafsi na Kampuni ya simu vilivyoendesha kwa ufanisi mkubwa zoezi la kuchangisha pesa zilizowasaidia waanga wa yale mafuriko. Hii yaonyesha nguvu za ndani ya nchi zinavyoweza kufanya maajabu.

Serikali hamuoni nguvu za wananchi????????

Friday, February 19, 2010

MIGONGANO YA USTAARABU NAMBA 2

VITUKO simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.

Baada ya kufika umati wa watu walimshuhudia hausigeli huyo akiwa ameshikwa na butwaa na walipomhoji alidai kuwa amechukua nguo za ndani za msichana wa mwenye nyumba huyo, Bhoke Naftal, ili azipeleke kwa bibi yake anataka kumuua kwa kumuweka msukule.Kutokana na kauli hiyo mwenye nyumba hiyo ambao ni Wasabato walianza maombi ndipo hausigeli huyo aliyefikia nyumba hiyo Desemba 24, 2009, alipoanza kujieleza mambo mbalimbali anayoifanyia familia hiyo kwa kushirikiana na bibi yake anayeishi kijiji cha Kitete mtaa wa Yangeyange Morogoro.

Hausigeli huyo alidai kuwa tangu afike katika nyumba hiyo bibi yake amekuwa akija usiku na hutembelea vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuichezea familia nzima.Amesema kazi hiyo aliinza tangu akiwa na umri wa miaka minne ambapo mafunzo hayo aliyapata kwa bibi yake ambapo tangu aanze amefanikiwa kumuua mtoto mdogo wa miaka miwili wa tajiri yake mmoja anayeishi Morogoro ambaye hadi sasa wamemuweka msukule.Ameongeza kuwa alimuua mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miezi mitatu ndani ya nyumba hiyo.

Baada ya kukiri kufanya kitendo hicho, wanafamilia ya mtoto huyo walimpiga na kumtimua kazi bila ya kumpa hata senti tano.Akizungumza na gazeti hili, hausigeli huyo amesema mara baada ya kufika katika nyumba hiyo bibi yake alikuja usiku na kumuomba damu ya Miriam Naftari (25), mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye alikwenda kumchukua Morogoro bila kumuaga.Amesema kuwa usiku huo alijitahidi kumnyonya damu dada huyo aliyekwenda kumchukua lakini jitihada zilikwama kwa kuwa dada huyo alikuwa ameokoka.Kutokana na hali hiyo, bibi akaamua achukue nguo za dada mkubwa wa familia ya Mzee Naftal ili wamtoe kafara ambapo ilitakiwa afe jana ndipo aliamua kuchukua nguo ili amkabidhi bibi yake huyo.Msichana huyo amedai kuwa akiwa kwenye maandalizi hayo ndipo Miriam alipogundua kisha kupiga kelele kabla ya yeye kutimiza azima yake.

Kwa hiyo familia iliamua kuchukua uamuzi wa kumfikisha kituo cha Polisi Stakishari kwa ajili ya hatua zaidi ambapo kulifunguliwa kesi namba STK/RB/ 2520/2010 iliyoripotiwa jana.Akizungumza na gazeti hili, baba wa familia hiyo, Mzee Naftal, amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa familia hiyo ni ya watu wenye kumcha Mungu kwani tangu hausigeli huyo afike katika nyumba hiyo kulikuwa na mabadiliko ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na homa za watoto zisizokwisha.Amesema kuwa wakati mwingine walikuwa wakilazimika kukesha kwa ajili ya maombi kutokana na kuchoka na vituko vinavyotokea mara kwa mara usiku. “Kwa kweli ilikuwa ni hali ya kutisha kwani kila baada ya siku mbili mtoto anaumwa mara huyu kesho huyu lakini hatukuacha maombi ambayo ndiyo yametoa majibu,” amesema.Habari hii itaendelea kesho ambapo tutawaelezea zaidi kuhusiana na namna ambavyo hausigeli huyo alikuwa akiifanyia familia hiyo na pia jinsi alivyokuwa akitumia ndumba na utaalam wake wa kurusha ndege hewani usiku.

Wednesday, February 17, 2010

MIGONGANO YA USTAARABU

Kinachojiri hapa Dar Es Salaam ni stori ambazo mie ninayeishi katika nguvu za mwanga 'enlightment' ninapata taabu sana kuziamini. Lakini kwa kuwa jamii inayonizunguka inazipigia upatu napaswa niendane na jamii hii.

jana kwa majibu ya radio clouds ( dar es salaam fm station) ni kwamba pale katika daraja maarufu la salender kumeonekana mambo ya ajabu. Mtoa taarifa ameshindwa kusema tukio hili lilitokea lini jambo ambalo linazidi kutuchanganya wanajamii. Eti mwanamke mmoja alikuwa kwenye gari akisubiria foleni kwenye mataa. Akatokea ombaomba akiomba msaada. Mwanamama huyo akashusha kioo na kutoa msaada wa pesa. Alaaaaah! ghafla mkono wake ukaanza kutoa manyoya ya paka na huku ukawa unavimba. Mwanamke huyo akamuuliza yule ombaomba nimekukosea nini? mbona mkono wangu unabadilika? Yule ombaomba hakujibu. Kwa kuwa traffic warden alisharuhusu magari na yule mama akawa anachelewesha foleni alichokifanya yule warden ni kumfuata yule mama na kumuuliza kulikoni?? mbona haundeshi gari? Yule mama akamuonyesha mkono ulivyovimba na kumueleza umeanza kuvimba na kubadilika alipotoa msaaada wa pesa. Traffic warden akamuuliza ombaomba imekuwaje??? Ombaomba akasema mkono utapona pale ambapo mwanamke yule atambusu. Toba!!! mwanamke akatoka ndani ya gari na kumbusu yule ombaomba. Alipombusu tu, wote wakayeyuka!!!!!!!!!!! salala.

Tena, siku tatu zilizopita, Radio Clouds ikatupa nyingine kali; katika kipindi chake cha jioni maarufu kama JAHAZI, kikiendeshwa na watangazaji wawili mahiri, Gadner Jihabeshi na Efrahim Kibonde wakisoma magazeti ya jioni walisoma habari moja kutoka gazeti la Dar Leo nalo likitoa mauzauza. Eti, mfanyakazi wa ndani ( Maid) alikutwa na mwajiri wake usiku wa manane akiwa uchi wa mnyama chumbani kwake huku amekalia ndoo na kuongea lugha hisiolewekwa. ( Alikuwa anawanga).Mwajiri ikabidi aiamshe familia nzima na walipomdadisi akakiri kuwa bibi yake huwa anatembelea familia hiyo usiku akitokea Tanga na huwa anatumia ungo na kuja kuwachezea familia nzima( Haikuelezwa anawachezea kivipi!!!). Mdada huyo vile vile akakiri kuwa alishawahi kuua mtoto mmoja huko alipokuwa anafanya kazi kabla hajaja kwenye familia hiyo. Zaidi Baba mwenye nyumba alikiri kuwa huwa anajisikia uchovu kila aamkapo asubuhi. jamani jamii ya kitanzania inakwenda wapi??

Siyo zamani sana takribani miaka 100 iliyopita, waafrika tulivamiwa na wazungu ( hasa wamissionari) ambao kwa sababu walizozijua wao wakauita ustaarabu ( culture) wetu kuwa ni wa kishenzi na kishetani. Tulilazimishwa kuachana na ustaarabu wetu na kukumbatia ustaarabu wa kizungu. Dini ya kigeni ( kikristu na kiislamu), muundo wa kiuchumi, lugha ya kigeni ( ingawa watanzania tunapigana sana kukienzi kiswahili) nk nk. Miaka 100 baadaye bado mababu wanalia huko waliko. Bado hizo ambazo siye wa kileo tunaziita nguvu za giza zinaonyesha na kupiga kelele ya ukunga ' NA SIYE TUPO'.

Mwanazuoni Ali Mazrui katika kazi yake 'The Africans' ( Page, 11) anaandika na ninamnukuu

The ancestors of Africa are angry. For those who believe in the power of the ancestors, the proof of their anger is all around us. For those who do not believe in ancestors, the proof of their anger is given another name. In the words of Edmund Burke, 'People will not look forward to posterity who never look back to their ancestors. But what is the proof of the curse of the ancestors? Things are not working in Africa. From Dakar to Dar Es Salaam, from Marrakesh to Maputo, institutions are decaying, structures are rusting away. It is as if the ancestors had pronounced the curse of cultural sabotage.

Cha ajabu serikali yetu ya Tanzania yadai kwamba haiamini uchawi!!! ingawa wananchi wake na hata viongozi wake wanashabikia uchawi na ushirikina. Kwanini wanashabikia?? jibu ni kwamba uchawi na ushirikina ni sehemu ya mapokeo yetu, ni ustaarabu wetu. Hatuwezi kuachana nao. Tulishuhuudia mwaka jana ambapo watunga sheria wetu tena ndani ya BUNGE letu tukufu walipowekeana upupu( powder ambazo mkemia mkuu alishindwa kutambua ni nini) kwenye viti!!!!!!!!! mmhhhh

Kama serikali inakaa kimya na kutofuatilia kwa karibu ustaarabu wa wananchi wake, sehemu nyingine yenye nguvu sana na yenye ushawishi mkubwa kwa jamii haikai kimya. HII NI DINI. Miezi kadhaa iliyopita maaskofu wa kikatoliki walikutana Vatican na katika 'resolution' yao waliamua kwamba kila askofu achague padre atakayekuwa 'mtaalam' wa kushughulikia uchawi na ushirikina. Wakotoliki wanajua wazi kwamba ili waweze kuwa 'on top of the game' ni lazima wawashughulikie wachawi kwani wenzao walokole wanatoa mapepo; karama ambayo inawapatia waumini wengi.

Ajabu ni kwamba viongozi wetu mmoja mmoja wanatabia ya kwenda kuaguliwa lakini hawako tayari kuuweka uchawi na ushirikina katika sera na mipango ya kitaifa. Viongozi wetu wanataka kuunda sera na mipango yenye 'support' na pesa ya misaada kutoka kwa wafadhiri tabia ambao inaonyesha ni ubinafsi uliotukuka na ukosefu wa ubunifu.

TUSIDANGANYANE WATANZANIA
WENGI TUNAAMINI UCHAWI NA USHIRIKINA.

MIGONGANO YA USTAARABU