Monday, April 18, 2011

jamani mbona twalewa umasikini wakujitakia??

Watanzania twalewa; tuwaangalie wenzetu waganda walioamua kuandamana wakipinda kupanda kwa gharama za maisha. Sisi twakubali tu, bora liende!!!

Wanauchumi wanasema huku kupanda kwa bei ya vitu hakuletwi na nguvu ya soko; bali kuzimwa kwa soko, ( market distortion).Kinachotokea watu wanaiba pesa za umma na kuweka pesa nyingi za nchi mikononi mwa wa wachache; ni hao watu wachache wenye pesa zetu wanapandisha bei za bidhaa. Wanaweza kusomesha watoto shule, tena shule za binafsi hata bei iwe kubwa vipi!! wanaweza kujenga majumba ya kifahari hata pale wanapopewa gharama zisizokuwa asilia.

jamani tuandamane!!! nani ananiunga mkono?

Saturday, April 16, 2011

UMUHIMU WA HESABU

ulishawahi kufikiria na kujiuliza umuhimu wa namba katika maisha yako ya kila siku.
1) Asubuhi unaamshwa na 'alarm' ya saa iliyoandikwa namba

2) unaangalia saa yako na kuizima na kuendelea kulala
Baada ya muda alarm hiyo hiyo iliondikwa namba inakusumbua tena

3) Unaamka na kabla ya kuondoka unabonyesha microwave iliyo 'display' namba na kupasha moto weetabix

4) halafu unavaa viatu viliondikwa namba 9

5) Halafu unaingia na kuwasha gari yenye 'speedometer' zilizoandikwa namba

6) Unasafiri na baadaye unafika nje ya ofisi yako na kusogelea kibox kinaitwa 'teller machine' kilichoandikwa namba

7) Kimashine hicho kinatoa noti ambazo zimeandikwa namba na unazihesabu kwa kutumia namba

8) Unaingia ofisini na bosi wako anaangalia kidude mkononi mwake chenye kuonyesha namba, tunakiita saa na anakupigia kelele kuwa umechelewa.

9) Kisha unapokea 'handover' kutoka kwa mwenzako kwenye karatasi iliyosheenezwa namba, wenyewe mnaita takwimu.


10) Unagundua simu yako ya mkononi aina salio na unamuita tarishi unampatia noti iliyoandikwa namba aende nje akakuchukulie 'voucher'. Anakuletea voucher na kisha unakwangua na kukuta namba. Unaziingiza hizo namba kwenye simu yako na kuruka hewani.

List haitaisha ni mwendelezo mrefu sana.

Hii yaonyesha kuwa toka enzi hizo namba zimetawala Dunia.

Husimnyime haki yake mwanao kwa kutomfundisha hesabu.Wanaojua kuchanganya changanya hizo namba na kutoa logic ndio wanaondesha ulimwengu.

Tafakari, Chukua hatua, Haki Elimu.

Thursday, April 7, 2011

mtukwao: LEADERS CLUB BONANZA; WATEULE MNATUANGUSHA

mtukwao: LEADERS CLUB BONANZA; WATEULE MNATUANGUSHA

LEADERS CLUB BONANZA; WATEULE MNATUANGUSHA

Wateule wa kipato cha kati mnakataa historia? Si mlisoma historia jamani!!! wapi matumizi ya historia ya Mkwawa mliyofundishwa na wazee wenu. Au mnawakufuru.

Tunaambiwa kuwa hivi karibuni kutakuwa na Bonanza pale Leaders Club ambapo mashabiki wa timu kali za Ulaya watachuana na kuwaonyeshana 'ubabe' wa kisoka. Ingawa ni muhimu kwa binadamu wa kawaida kufanya mazoezi na kupasha misuri, ninachokataa ni ajenda inayotumika katika kupashana misuri hapo Leaders Club.

Wanaendesha bonanza hili ni kundi la watu tunaowaita 'wateule'( intelligensia) au kwa lugha ya kuazima wanaitwa 'Middle class'. Sasa katika hizi dhama za harakati ya kimapinduzi kama inavyoshuhudiwa Libya, Algeria, Misri na kwingeneko, kwa kweli hatutakiwi kushangaa na kuwa na starehe hii tuliyonayo. Jamani, tuulizane sisi wateule tulio Dar Es Salaam tunashindwa kuungana nguvu zetu na kufanya mabonanza ya kimapinduzi? Tukumbuke hizo timu tunazoshabikia za Barcelona, AC Milan, Manchester, nk zimeundwa baada ya wananchi wa nchi hizi kupigania mapinduzi ya ukweli mpaka wakawa na demokrasia ya ukweli yenye kuwapa utu wananchi wao.

Ikimbukwe 1848 kulikuwepo na mapinduzi ya uhakika Ufaransa, Uhispania na Italia, mapinduzi yaliyoweka mbegu ya hizi timu tunazoshabikia kibudu kibudu. Tunaijua historia ya AC Milan, au tunapiga makelele kwenye luninga kizembe zembe tu?

Kwa kushindwa kuwaangunisha wakulima wa vijijini katika vita ya kuungoa UFISADI ulioshamiri; tunawasaliti watemi wetu akina Mtemi Mkwawa!!!

Tuamke wanasheria, wasomi wa mlimani, wahandisi, na madktari, mapinduzi ya Misri, Libya, yanaletwa na makundi haya. Sie twapiga kelele za Mau U

OLE WETU.