An empty stomach is not a good political advisor!!!
Source 'The Guardian' ( Tanzanian daily)
Saturday, October 31, 2009
ZA MWIZI AROBAINI, HAPANA ZA MWONGO.....
Wanasiasa 40 walipata ajali mbaya sana porini,na baada ya ajali hiyo alitokea mkulima mmoja na alipoona hivyo alichimba shimo kubwa na kuwazika wote kwa pamoja.Baadaye polisi walikuja eneo la tukio na kumkuta huyo mkulima na kuanza kumhoji kuhusiana na ajali hiyo.
Mahojiano yalikuwa hivi:-
Polisi :-
Uliona ajali jinsi ilivyotokea?
Mkulima :-
Hapana, nilikuta imeshatokea na maiti zimezagaa..
Polisi :- Zipo wapi maiti?
Mkulima :- Nimezizika
Polisi :- Una uhakika wote walikua wamekufa?
Mkulima :- Kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo!!!mi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote....

Tuesday, October 27, 2009
FAITH APATA KOMUNIO YA KWANZA
Baada ya mafundisho ya mwaka mmoja, Faith Nyamwocha afurahia matunda ya somo la kikristu pamoja na familia yake. Waliopitishwa kupata sakramenti hiyo ni 6 kati ya watoto 30. Wengine 24 walishindwa kudhibitisha kuwa walishapata ubatizo. Kwa wakristu huwezi kupewa komunio ya kwanza kabla ya kubatizwa. Natamani 'discpline' hii ingekuwepo katika taasisi za serikali ya Tanzania.
Sunday, October 25, 2009
KURA YA NINI? SERIKALI NI MFU!!!
Jumapili iliyopita watanzania kote nchini walitarajiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa katika ile hali ya kutimiza haki zetu za kimsingi za kikatiba, yaani kuchaguliwa ama kuchagua viongozi tunaotarajia watatuletea maendeleo katika vitongoji vyetu.
Kwa mujibu wa Waziri wa nchi anayeshughulikia serikali za mitaa, Mheshimiwa Celina Kombani namba ya waliojiandikisha kupiga kura nchi nzima ni sawa na 53% ya watu millioni 16.1 ambao serikali ilikadiria wangejiandikisha kupiga kura.
Uchaguzi umeisha salama na umefanyika katika vituo 66,136 vilivyoko katika vijiji 11,197 na mitaa 2,606 katika halmashauri 132 nchini, ambapo viongozi 279,925 wamechaguliwa katika ngazi ya vijiji na vitongoji, na 15,636 katika ngazi ya mitaa.
Chama Cha Mapinduzi, CCM kimeibuka na ushindi mkubwa ambapo kwa mkoa wa Dar Es Salaam wajumbe 34 walipita bila kupingwa ambapo mkoani mbeya wajumbe 4000 wa CCM kati ya 5,592 vile vile nao wamepita bila kupingwa.
Licha ya haya yote mimi mkazi wa Tegeta, Dar Es Salaam sikupiga kura, wala sikujua sehemu iliyokuwepo kituo cha kupigia kura.
Sababu ni nyingi lakini zaidi ni ule ukosefu wa mwamko wa kisiasa siyo tu kwa mimi kama mtanzania bali pia kwa watanzania wenzangu ambao niliwaona wakiendelea na maisha yao ya kila siku pale mtaani kwangu. Kuna waliokuwa kwenye maduka yao ingawa hii ilikuwa ni siku ya kumwabudu Mungu kwa walio wakristu, kuna niliowaona wakibeba ndoo za maji kichwani wakiangaika kutafuta maji, kwa wale wakulima niliwaona wakimwagilia michicha yao,na waangaikaji wengine niliwaona wakisukuma mikokoteni. Jirani yangu aliendelea kusimamia mafundi wanaomjengea nyumba yake. Kwa kifupi wengi hatukustuka na uchaguzi huu.
Waziri Kombani alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari siku mbili kabla ya uchaguzi alikiri kuwepo na idadi ndogo ya watanzania waliojindikisha kupiga kura. Alisema kuwa wengi waliojindikisha ni wananchi wa vijijini ambapo 30% walijiandikisha ambapo maeneo ya mijini namba ilikuwa ya chini zaidi. Akaainisha kuwa sababu mojawapo ya idadi ndogo ya wapiga kura maeneo ya mijini ni uelewa mdogo ( ignorance) wa watu wanaofikiri kuwa uchaguzi hauna manufaa kwao. Vile vile Radio ya binafsi yenye makao yake makuu jijini Dar Es Salaam, Clouds Fm ilitoa takwimu ya watu 500,000 waliopiga kura katika jiji la Dar Es Salaam kati ya wakazi wa jijini.
Lakini mie naona ni ukweli kuwa uchaguzi hauna maana hasa kwa mtu wa kawaida kwani hakuna kitu anachoweza kujivunia kuwa ni kazi ya viongozi aliyewachagua katika uchaguzi uliopita. Wananchi hawategemei barabara zijengwe na viongozi wao hapa mitaani mwetu, wala hatutegemei kujengewa kituo cha polisi karibu na makazi yetu bila kuweka nguvu zetu wenyewe, wala hatuwaambii wajumbe wa mitaa yetu wakusanye takataka kwa niaba yetu. La hasha! wananchi kwenye vitongoji wanakosa viongozi wa kuwahamasisha, wanakosa viongozi wa kuwaongoza, viongozi watakaoonyesha njia ya kuelekea kwenye maendeleo ya kweli. Tunaliliona kwenye mitaa na vitongoji vyetu ni viongozi bubu, wasiotoa maelezo yenye tija; na tunapofika hapo nchi inakuwa inaingia kwenye mashaka sana. Viongozi wanadharaurika na kila mtu anachukua uamuzi kwendana na mazingira yake.
Katika nchi yenye mtazamo makini, wananchi wanatarajiwa kuilinda na kuitetea katiba yao, na upigaji kura ni njia sahihi ya kutimiza adhima hii. Mwalimu Nyerere ( Nyerere 1995) aliwahi kuandika kuwa wakati wote wananchi wanaweza kuitetea katiba kama wanajua wakati wote wawakilishi wao wanafanya nini kwa niaba yao. Kama hawaambiwi ukweli kinachotokea ndani ya nchi yao wananchi hawa watawezaje kuitetea katiba?
Hapa kwangu Tegeta na sehemu nyingi za Dar Es Salaam ni kila mtu na lwake! mtu anachoweza kufanya yeye kama mtu binafsi anakifanya bila kushirikishwa au kuhamasishwa na kiongozi wake wa mtaa. Ninapoamua kujenga ukuta kwenye nyumba yangu hii inamaana ninajiwekea kizuizi na jumuiya inayonizunguka. Ninapoweka simtank la maji ya ziada ina maana sitarajii na wala sitalalamika pale DAWASCO watakaposhindwa kunipatia huduma ya maji. Ninaponunua LandCruiser, na kulipitisha kwenye barabara mbovu iliyojaa mashimo mfano wa mahandaki ina maana sitarajii mwenyekiti wa serikali za mitaa kuitisha mkutano wa wananchi kujadili njia mbadala ya kuweka vifusi kwenye barabara za vitongoji vyetu. Wazungu wanasema 'Its a private solution for the public problem'
Fanon(1963, p. 119) analielezea tabaka la wasomi ambalo baadhi yao linajiingiza kwenye siasa kama ifuatavyo;
Inaonekana kwamba tabaka la wasomi halijajiandaa, wala halina uhusiano au ukaribu wa kimatendo ( practical) na umati wa watu, ule uvivu wa hili tabaka la wasomi, na uwoga wao katika muda muafaka wanapotarijiwa kutimiza majukumu yao ya kimapigano huleta hasara kubwa kwa jamii.
Hata baada ya miaka zaidi ya 40 tangia tupate uhuru, mapigano ya sasa siyo yale ya kumuondoa mkoloni, bali vita ya sasa ni kuuondoa ukoloni mamboleo unaokuja kwa sura ya utandawazi ( globarization). Lakini kama vile anavyoanisha Issa Shivji (2007) viongozi wanaoshika madaraka nchini kwetu wanaimba wimbo wa ukoloni mamboleo badala ya kuupinga wakiwa bega kwa bega na wapiga kura wao.
Kiongozi wa mtaa ninaemtaka mimi ni yule atakayetambua kuwa mipango ya ukoloni mamboleo ndiyo iliyosababisha bei zetu za mazao vijijini kushuka bei mno hivyo kulileta kundi kubwa la vijana mjini. Ni kiongozi atakayekuja na mipango endelevu ya kulipa ajira jeshi hili la vijana ndio atakayenifanya nipige kura ya kumchagua.
Kiongozi ninayemtaka mimi ni yule atakayetambua kuwa elimu inayotolewa na serikali ni afifu mno hivyo kuja na mipango inayowashirikisha wananchi wa mtaani ambao wote wanapenda watoto wao kusoma shule katika mipango ya kujenga maktaba, au shule ya kisasa.
Serikali yetu imekufa! a stateless society!!! No police, no healthcare, no fire brigade, no proper public schooling, no adequate water supply, infrequent power supply, and above all no effective leadership.
Mungu Ibariki Tanzania.

Saturday, October 24, 2009
Fatiki ya Rwanda
Chanzo cha BBC swahili service kinatutaarifu kuwa nchini Rwanda, serikali ya Mjeshi Kagame imeamua kufanya tathmini kwa wafanyakazi wake wa serikali kila mwezi, ambapo alama kama zile za shule zitakuwa zinatolewa kwa watumishi wa Umma.
Chanzo hicho kinatutaarifu kuwa mtumishi wa umma atakayepata alama kati ya 70-100% ataendelea na kazi na ikiwezekana atapandishwa cheo. Alama 50-69% atasimamishwa kazi na kupewa nafasi ya kutuma maombi ya ajira upya, ambapo yule atakayepata chini ya alama 50% anafukuzwa kazi.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumishi wa umma kuwa wale viongozi wa vitengo vya serikali ambao ndio wanaotoa hizo alama wanaweza kuwa na visasi na waajiriwa hivyo kutoa maamuzi ya upendeleo, ( Victimization).
Wewe hii unaionaje?
Watumishi wa serikali ya Tanzania wamekuwa na tabia ya uzembe, ubadhirifu, ulaji wa rushwa na kwa ujumla kuwajibika kumekuwa kwa mashaka sana. Nakumbuka miaka ya 1990's Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliwahi kutangaza upitishwaji wa Fagio la chuma kwa watumishi wazembe. Vile vile miaka hiyo hiyo aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, mpiganaji Augustino Lyatunga Mrema alianzisha tabia ya kuvamia ofisi za serikali na kuondosha viti vya mtendaji aliyekuwa hayupo kazini.
Licha ya juhudi hizi za zima moto? bado watumishi wa serikali wamekuwa wakifanya kazi kimazoea, kusuasua na kivivu.
Tanzania, tufanye nini?

Friday, October 16, 2009
NI UMASKINI WA MAWAZO SIYO HALISIA
Leo Dunia inatubeza siye wa nchi 'maskini' kwamba ni sikukuhuu yetu! Inaitwa siku ya umaskini Duniani. Kiukweli siye wa nchi za ulimwengu wa tatu siyo maskini bali umaskini wetu ni wa mawazo tu. Viazi vitamu vinakubaliana na hali ya joto hivyo kwa akili ya kawaida vingetakuwa viwe vinatawala kwenye meza zetu kama sehemu ya kifungua kinywa. Ila kwa sababu tunapenda sana kuiga chakula wanachokula wale waliotutawala basi tunaona vyetu ni vya kishenzi. Watawala walipokuja na mkate na siagi tukaona viazi vyetu havina mpango. Wahaya wanaita viazi vikuu, ebitakuli, maana yake ni Hivi weka pembeni. Kuna stori kwamba muhaya mmoja alipowekewa vyakula vingi mezani alichagua vyakula vingine na kuachana na viazi vikuu.
Leo hii husipokula mkate na siagi unaonekana umeishiwa na watoto wa mjini wanasema 'umefulia'. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya vitafunwa vinaagizwa kutoka nje ya nchi hivyo tunapoteza pesa zetu za kigeni. Weetabix inatoka Uingereza na siku za baadaye itachukua nafasi ya mkate.
Msomi ninayependa kusoma kazi zake Ali Mazrui katika kitabu kinachoitwa 'The Africans' aliandika, ninamnukuu katika lugha ya kiswahili.
Katika kipindi cha kizazi kimoja kilichopita tumeshuhudia kasi kubwa ya waafrika kuiga mila za kigeni na ufuatiliaje wa maisha ya ughaibuni. Kama wayahudi waliokimbilia nje ya nchi yao wangediriki kubadilisha ustaarabu wao kwa haraka kama waafrika wanavyofanya ndani ya nchi zao, maajabu ya utambulisho wa kiyahudi yasingedumu katika millennia mbili au tatu walizokaa mbali na nchi yao. Hata sasa waafrika wengi wanaonekana kubadilika kwa kasi kubwa kiutamaduni katika kizazi kimoja zaidi ya wayahudi walivyobadilika ndani ya miaka 1000 nje ya nchi yao.
Mchele unaliwa dunia nzima, lakini muhogo ni wakwetu, wakwetu asilia. Zao la muhogo linaweza kuchemshwa, kuchomwa, kubanikwa, kukaangwa, na kupikwa kama chakula cha mchana. Vile vile muhogo unaweza kukobolewa na kupatikana unga mtamu wa ugali, tunaweza vile vile kunywa uji wa muhogo na hivyo kuachana na weetabix. Majani ya muhogo maarufu kama kisamvu ni chakula kinachodharauriwa na watanzania hasa wa mjini eti ni mlo wa kimasikini.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda alituasa watanzania tuache kuwa na kasumba ya kupenda mchele na unga na kuacha mazao yanaostahimili ukame kama mihogo. Tumekariri kuwa mchele na unga kuwa ni vyakula vikuu na hata wakati mwingine ukame unavyokamata tunaagiza nafaka hizi kutoka nje ya nchi na kutumia pesa chache za kigeni tulizonazo. Inasikitisha tunapoona wachaga hawali mihogo kwa ujinga tu kwamba zao hilo ni sumu. Ni ujinga vile vile kuwaona wahaya wanakufa njaa eti kwa kuwa ndizi zimeingiwa na wadudu. Inauma kuona wahaya wanakosa pesa ya kujikimu eti kwa kuwa kahawa imekosa soko duniani. Kwanini wahaya wasilime mihogo na kuwauzia wakazi wa mijini wanaopoteza pesa kuagiza weetabix?
Waafrika tumekuwa watu wakusaidiwa kiuchumi na hata kimawazo, tuchukulie mfano wa tajiri mkubwa mmiliki wa Microsoft, Bill Gates aliyezindua hivi karibuni mpango wake wa kilimo endelevu kinachozingatia mazao ya nyumbani ili kunusuru Bara la Afrika na janga la njaa. Mpango huo utakaogharimu dollar million 120 unalenga kutuelimisha waafrika umuhimu wa kupanda mazao kama viazi vitamu ambavyo vinasifika kutokomeza mapungufu ya Vitamin C hasa kwa watoto.
Mawazo endelevu na yenye nuru ya Gates yanaungwa mkono na Dr Hartmann, Mkurugenzi wa shirika la kitafiti linalotafuta ufumbuzi wa njaa na umaskini wa kiafrika liitwalo IITA. Kwenye mahojiano na The Guardian, 17 of October, mtafiti huyu anatoa angalizo kwamba walaji wa kiafrika inabidi wasaidiwe kujifunza kubadilisha jinsi wanavyokula ili wasiwe wanategemea mazao machache. Anaanisha kwamba nchi zilizoadhirika zaidi na njaa ni zile zinazotegemea mchele, mahindi na ngano mazao ambayo ni maarufu katika soko la dunia. Wakati mazao hayo yamekuwa yakipanda bei siku za hivi karibuni, bei za mazao kama mihogo na viazi vikuu vimekua vikiwa na bei hisiyoteteleka.
Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa septemba 29 na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na utafiti wa sera za chakula IFPRI yenye makao yake Washington, Marekani inahasa kwamba ifikapo 2050, Afrika kusini mwa jangwa la Sahara itapungukiwa na mavuno ya mchele kwa 14%, ngano 22% na mahindi 5%. Mapungufu haya yatakayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yatazidisha hali ya utapiamlo hasa kwa watoto.
Thursday, October 15, 2009
NI WIKI YA KUJISOMEA
Nani kasema watanzania hatupendi kusoma? hapa ni asubuhi maeneo ya Mwenge kituoni. Kama walivyo mabosi, mtanzania wa kawaida anapenda kujua nini kinaendelea katika nchi yake. Survey hii nilivyoifanya mchana nilikuta 'newstands' zikiwa hazina watu wanaopiga 'chabo' kama ilivyo asubuhi. Pale mwenge nilizubaa kwa muda hiyo asubuhi na niliweza kushuhudia wapitia njia wakisoma gazeti bila kununua. Wazungu walisema, 'do not read a book by its cover'. Viongozi wetu wanaposiliana na wananchi kupitia vyombo vya habari hususani magazeti ujumbe wao hauwafikii walengwa kwa muda husika na hali hii inafanya wananchi wasiweze kujua kinachoendelea ndani ya nchi yao wenyewe.
Sababu kubwa inayofanya 'wadanganyika' kushindwa kusoma 'morning news' ni ukosefu wa kipato kwani kwa wastani bei ya gazeti ni 500/= wakati wananchi wengi tunaishi chini ya $1 kwa siku.
Ila kuna njia mbadala ya kuhakikisha kuwa siye wananchi tunapata habari kila siku na hivyo kujua viongozi wetu wanatuambia nini au wanafanya nini. Kwanini tusiwaige wazungu mambo ya maana badala ya kuiga vitu vya kipuuzi. Mfano nchini Uingereza halmashauri za miji zinachapisha na kusambaza magazeti kwa wakazi wa miji bure huku makampuni ya miji hiyo yakigharimia magazeti hayo kwa kutangaza matangazo. Kwa kufanya hivyo wananchi wanapata habari ya kinachoendelea katika miji yao na wakati huo huo halmashauri za miji zinapata faida na kuwa na pesa za kuendesha miji.
Tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wanatarijiwa kupiga kura huku wakiwa 'mbumbumbu' bila kujua mipango ya viongozi wao. Ama kweli wajinga ndio waliwao.

Tuesday, October 13, 2009
WAAFRIKA WA 'BLING BLING'
wakata miwa
Monday, October 12, 2009
TUCHANGIE KANISA KATOLIKI TEGETA
Ndugu zangu wapendwa! waumini wa hapa kitongoji changu cha Tegeta tunajenga kanisa kama linavyoonekana kwenye taswira hii. Tunaomba mtusaidie kuchangia kwa kushindania bahati nasibu lukuki ikiwemo zawadi ya Gari jipya la kijapan liitwalo Toyota Spacio. Bei ya tiketi moja ni sh. 2000/=. Tafadhali sana naomba tuwasiliane kwa namba +255 712378647 nikuuzie tiketi yako. Hima tujenge nyumba ya Bwana.
Kristu! Tumaini letu.
Kristu! Tumaini letu.
Mji wa Moshi! Ni msafi sana
umeshawahi kufika mjini Moshi, Tanzania? Nilisoma elimu ya sekondari nje kidogo ya Moshi miaka 1980's. Hapo ni roundabout ya KNCU. Mdau Kidato Mbwana ambaye ni mwenyeji wa Moshi, aliishi uingereza kwa takribani miaka 9. Juzi alirudi kwao Moshi, na mandhari ya usafi haliyoaacha wakati huo alikuta mambo mswano kama alivyoacha.
Tuesday, October 6, 2009
JANA ILIKUWA SIKU YA MAKAZI DUNIANI
Jana 5th of October ilikuwa ni siku ya makazi duniani; lakini pale eneo la kimara nje ya jiji la Dar es salaam kanisa katoliki lina ugomvi wa kiwanja na shangazi yangu. Kihistoria kanisa lina jadi ya kupanuka, hulka hii ilikuwepo tangu enzi ya Mt. Paulo alieneza injili siyo tu Jerusalem bali pia nje ya mitaa yake na kuelekea Cypress, Pamphylia, Pisidia, and Lycaonia, na sehemu kubwa ya Asia. Vile vile alieneza injili Pisidian Antioch, Iconium, Lystra, and Derbe. Kanisa linataka kumpatia 34m/= takribani $28,000, pesa ambayo hawezi kupata nyumba yenye dhamani ya nyumba yake. Mmh hili ni jina la Bwana hama la shetani?
Shangazi ana hati mkononi, lakini kanisa bado halijatuonyesha hiyo hati yao wanaodai wanayo.

On Enviroment; Kagera iko juu!
On recycling Kagera tuko juu! wala hatuhitaji semina na makongamano. Wahaya utumia majani ya migomba kufungia kahawa.( kahawa ni kama wine ilivyo kwa waingereza). Halafu baada ya kufungua majani hayo urudishwa tena migombani kama mbolea. Tukitoka huko vijijini na kuja mijini tunakuja na akili hiyo hiyo ya shambashamba na kutupa ovyo takataka. Matokeo yake ni aibu tupu! Uchafu wa hiyo picha ya hapo juu ni mitaa yangu ya Tegeta, Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)