Thursday, January 28, 2010

MFUMO UMEMUUA SWETU FUNDIKIRA

Wiki hii vyombo vya habari vya Tanzania vimegubikwa na taarifa ya mauaji ya kusikitisha ambapo kijana mmoja aitwaye Swetu Fundikira alipigwa na hatimaye kupata majeraha yaliyomsababishia kifo mara pale alipokimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam. Taarifa zinafafanua kwamba wanajeshi watatu waliokuwa wanatoka katika kumbi ya starehe walighazibishwa baada ya gari lao kuchunwa na gari la Sweti. Kilichofuata ni kipigo cha uhakika.

Vifo kama hivi vimekuwa ni kawaida sana ingawa misiba mingine inakuwa siyo rahisi kumngamua muuaji kutokana na mazoea ya mfumo wetu tuliozoea. Kwa waafrika 'kifo' ni suala nyeti sana ( sacred) na jamii yetu haitoi nafasi ya kuzungumzia chanzo cha kifo. Kwa kuwa kifo ni majariwa ya mwenyezi Mungu na wala hatuna upeo wa kuzungumzia ni nini chanzo cha kifo fulani, basi tunakaribisha vifo vingine kirahisi sana. Hata kama tutatoa lawama kwa wale wanajeshi, je tunajua umakini wa wahudumu na waganga wa pale Muhimbili katika zile harakati za kuyaokoa maisha ya marehemu? Je, Marehemu Swetu alitolewa pale eneo la tukio na usafiri wa aina gani? Sijafuatialia hili lakini nina wasiwasi kama gari lililokamilika la wagonjwa ( fully equipped ambulance) lilitumika katika kumsafirisha kuelekea Muhimbili. Tuwarudie wale maaskari; Nikisema kwamba hawakuwa na 'reference point' ya adhabu nyingine kali iliyotolewa na wauaji/ watesaji kama wao nitakuwa nimekosea?

Siku tatu kabla ya kifo cha Swetu, rafiki yangu alipata ajali ya pikipiki ambapo alilivaa 'truck' barabara ya morogoro majira ya saa mbili za jioni. Rafiki yangu hakuwa na 'helmet' na inasadikika kuwa alikuwa amekunywa pombe. Barabara ya moro kipande kile haina taa za barabarani, na wala lile lori halikuwa limewasha taa. Haya ndiyo mazingira yaliyomuua rafiki yangu, ni mfumo mzima na wala siyo majariwa ya mwenyezi Mungu. Nilipohudhuria msiba wa rafiki yangu, hakuna hata mtu mmoja kati ya watu waliopewa nafasi ya kutoa hotuba pale mazikoni aliyewaasa watu hasa vijana kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa. Pale msibani walikuwepo viongozi wa serikali za mitaa, lakini tulishindwa kuwaambia kuhusu umuhimu wa taa za barabarani. Waingereza wanasema, 'we should take the bull by its horns'.

Mwezi huu nilizika mke wa rafiki yangu ya mpenzi, kilichomuua? operesheni ya uzazi!!!!, cha kushangaza pamoja na majonzi makubwa tuliokuwa nayo, hatukuwa na muda wa kufuatilia kwa kina 'ni nini hasa kilichojiri kwenye chumba cha upasuaji'. Kufanya hivi siyo kumtafuta mchawi ila ni katika jitihada ya kujua chanzo kamili ili kuzuia misiba mingine ya ndugu zetu wapendwa.

Lakini kwa waafrika, hata ninapoandika hili naogopa kuonekana nakufuru kwani 'kifo' hakizungumziwi; KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA. We should call a spade a spade. Nakumbuka Nelson Mandela alipokuwa anamzika mtoto wake alisema wazi wazi, kuwa mwanae amekufa kwa ukimwi. Ila huku kwetu marehemu hasemwi vibaya.

TUNAJIUA WENYEWE NA KWA UHAKIKA TWAZIDI KUFA.

Monday, January 25, 2010

This is how it should be done!!!!

“Those who receive leadership privilege, have a duty to repay the sacrifice which others have made. They are like the man who has been given all the food available in a starving village in order that he might have the strength to bring supplies from a distant place’’

Friday, January 22, 2010

KUPANDA CHEO

Dear all sio mbaya tuka share hii kitu hapa, najua kwa wengine itawasaidia na wengine wataona mada ndefu sana wataipotezea,but pls take a time read this,who knows it might touch you and change the way you are working.


wengi tunapenda vyeo.Ndio hulka ya binadamu. Kuna kuridhika fulani kunakotokana na kuwa na cheo kikubwa.Wakati mwingine haijalishi hata kama cheo alichonacho mtu hakiendani na kipato anachopata.Anachojali yeye ni kwamba yeye ndio Rais,Mkurugenzi Mkuu,Mkuu wa Mkoa,Mwenyekiti,Meneja nk. Kila mahali pana vyeo…hata jela kuna mfungwa mkuu nk.
Kwa wengi,cheo humaanisha kuongezeka kwa kipato.Cheo humaanisha mazingira mazuri zaidi ya kazi.Kama alikuwa kwenye kajiofisi kadogo basi anajua akipata cheo ina maanisha kuwa na ofisi kubwa na pengine hata kitanda cha kupumzika akichoka achilia mbali kuwa na luninga ofisini na mambo mengine kede.
Sasa ufanyeje ili upandishwe cheo.Leo tutaangalia mambo 7 ambayo mtu anaweza kufanya ili kupandishwa cheo.Lakini kabla sijaenda mbali sana,naomba nikutahadharishe kwamba mbinu ninazokupa zisiwe ndio muongozo wako.Lazima ujivike uhalisia(naturality) kwanza. Mbinu hizi ni kukusaidia tu.Ukizifuata kwa kanuni mpaka ukajisahau kwamba wewe ni nani na unatoka wapi,utatumbukia shimoni.
Fanya Kazi Yako Vizuri: Najua kwa wengi hili linaonekana kuwa wazi.Kama hufanyi kazi vizuri basi huwezi kupandishwa cheo.Au sio? Jibu ni kwamba ingawa huo ndio ukweli wapo watu wengi ambao hawafanyi kazi “vizuri” na badala yake wanafanya tu kazi ili mradi siku iishe aondoke zake akasubiri mwisho wa mwezi apate mshahara.
Kwa bahati mbaya,waajiri na watu walio na mamlaka ya kukupandisha cheo huwa wanaona hili kwa urahisi sana.Ipende kazi yako,ipende kampuni unayofanyia kazi. Weka uadilifu na maarifa ya ziada katika kazi zako.Cheo kitakuja.
Onekana: Kisichopo machoni ni vigumu kuwepo moyoni pia.Huo ni msemo mzuri na unaoweza kukumbusha umuhimu wa kuonekana.Unapokuwa kazini hakikisha kwamba watu(hususani wakuu wako wa kazi) wanakuona na wanaona kazi unayoifanya.
Usidanganywe na mtu anayekuambia kwamba ukionekana onekana unakuwa kama unajipendekeza.Hapana.Kama wewe ni mtu wa kujifichaficha,inaonyesha wazi kwamba hujiamini na hivyo hata ukipandishwa cheo kuna ulakini kama utayaweza madaraka yako mapya.Kwa maneno mengine,ondoa soni.Onekana.
Jitolee: Upo mtazamo fulani kwamba kila unachokifanya kazini(hususani cha ziada au nje ya mkataba wa kazi yako) basi ni lazima kiambatane na ujira fulani.Huo ni mtazamo usiofaa sio tu kwa sababu hautokusaidia kupanda cheo bali hata kwenye maisha ya kawaida nje ya kazi.
Kama kuna mtu anahitajika kwenye idara yako kwenye kutoa maelezo fulani,mahali fulani bila hata malipo ya ziada,kuwa wa kwanza kujitolea kufanya.Mwenzako ana tatizo fulani la kikazi,msaidie.Wakati mwingine usingoje kuulizwa au kuombwa.Kuwa wa kwanza kuomba kusaidia.
Zungumzia Ndoto Zako na Wakuu Wako wa Kazi:Kuna nyakati ambazo ni muhimu kuzungumzia ndoto zako.Kama unataka kupandishwa cheo basi unaweza kabisa kuzungumzia ndoto hizo na wakuu wako wa kazi.Lakini kuwa makini usifanye hivyo kwa vitisho wala majibizano.Kwa weledi kabisa jadili ndoto hizi na wakuu wako.Unaweza kufanya hivyo kwa kuweka swali mezani kwamba nifanyeje ili niweze kupandishwa cheo?
Wakuu wengi wa kazi wanaelewa kuhusu ndoto za namna hii kwani hata wao walishapitia huko.Mara nyingi watakusaidia kutimiza ndoto zako.Ila kuwa makini usiongelee kuhusu kuchukua cheo cha mtu ambaye unamwambia ndoto zako.Anaweza akakuhujumu.
Husiana/Shirikiana Vizuri na Watu: Kushirikiana vizuri na watu kunakwenda sambamba na kuepuka migogoro.Kimsingi kuepuka migogoro ni matokeo ya mahusiano mema miongoni mwa watu(wafanyakazi).
Watu wengi wamepitwa na vyeo sio kwa ukosefu wa ujuzi au ufahamu katika kazi zao bali kwa sababu hawaonekani kuwa na uhusiano mzuri na watu au wafanyakazi wenzao.Kumbuka kwamba ninapozungumzia mahusiano mema kazini simaanishi umaarufu.Unaweza kuwa maarufu kazini kwa sababu labda baba yako ni mtu anayefahamika.Lakini kama hauna mawasiliano mema na watu,huaminiki na wala wenzako hawawezi kukutegemea katika kitu fulani,basi cheo nacho kitakupiga chenga.Epuka kujenga maadui,kuwa tegemezi,jenga mbinu nzuri za kuwasilisha kwa wenzako mawazo yako.
Changia Mawazo: Kila unapopata nafasi,changia mawazo chanya katika vikao au mazungumzo ya kawaida kazini. Jadili kwa uwazi na umakini jinsi ambavyo unadhani mnaweza kufanya ili kuboresha utendaji wenu wa kazi na hivyo kuleta faida zaidi. Wakuu wengi wa kazi(sio wote) hupenda kuona mtu ambaye ana mawazo chanya na ambayo anawaza kwa mapana na marefu. Hiyo sio tu sifa ya uongozi bali pia ishara muhimu kwamba ukipandishwa cheo,itakuwa kwa faida ya kampuni na pia wewe binafsi.
Jiwekee Malengo: Kama ilivyo katika maeneo mengine ya kimaisha,ni muhimu kuwa na mipango na malengo madhubuti. Kama unataka cheo zaidi au malipo zaidi basi usisite kujiwekea malengo.
Unaweza kusema kwamba nitafanya kazi katika kampuni hii kwa miaka mitano ijayo.Ukiona miaka mitano imefika na hakuna hata dalili za mambo kubadilika,kubaliana na matokeo na nenda aidha kutafuta ujuzi zaidi au kubadilisha muajiri.Usijisikie vibaya kushindwa kufikia malengo yako.Kumbuka haijalishi umeshindwa namna gani bali unachokifanya baada ya kushindwa.
Mwisho kumbuka cheo ni dhamana.Unapofikia malengo yako na kupata cheo unachokitaka,kumbuka kutotumia vibaya madaraka uliyopewa.Bila shaka umeshaona jinsi ambavyo watu mbalimbali maarufu duniani wameporomoka kutoka katika ngazi ya vyeo waliyokuwa wameipanda kwa taabu na muda mwingi kutokana na kashfa za matumizi mabaya ya madaraka.
thanks wadau,ni elimu tu tunapeana bure kabisaa.

Friday, January 15, 2010

USHAURI KWA MAKAPERA KUTOKA KWA MDAU GRACE

Hi! Mtukwao!1)

Hakuna umri wa kuoa, ingawa unatakiwa uoe ungali kijana (nguvu) ili kama Mungu atawajalia watoto uwe na wakati mzuri wa kuwajengea msingi wa maisha.

2)Kuoa ni ili kusaidiana kimwili, kimawazo, (kuwa kitu kimoja) na kujenga familia, (kupata watoto) hapo simaanishi kuwa mkioana ni kila mtu anabahatika kupata mtoto au watoto ila ndio tegemeo la wanandoa wengi.

3) Kumuoa nani ni chaguo la mtu mwenyewei.Unamuoa unayempenda au mnayependana ii.mwenye mtavumiliana kwenye shida na raha, *(lako langu, langu lako.)iii. Mtakayeheshimiana (respect matters).

4) Majuto yapo hasa pale utakapogundua kuwa mwenzako mnatofautiana kitabia au hali yoyote ile ambayo inawezafanya mtu akakwazika. i) Kuna mtu unamuoa hujui alikupenda kwa ajili gani pengine kama ni wakati mlikuwa vizuri, akaona umamfaa bila kujua maisha ni kupanda na kushuka leo unacho kesho huna, ninamaana kwamba, kuna wengine hawavumilii shida. Hapo basi ndio hasira zinaanza, kiburi na kutosikilizana. ii) Tabia zako ambazo sio nzuri ulijaribu sana kuzificha na sasa unaziweka azarani yaani hujifichi tena, pia inaleta majuto. Nafikiri nikisema tabia mnanielewa maana hata zingine zimepelekea ndoa nyingi kuvunjika.iii) Kutopata mtoto/watoto inaleta shida pia kama nilivyoekezea kwenye namba mbili mategemeo ya wengi ni kupata familia.iv) Kweli kuna watu wanaoa au kuolewa just a record hajui wajibu wake.

5) Furaha huwepo kutegemeana na nyie wenyewe mnavyoendesha maisha yenu. Hilo nawaachia wanandoa.

Flory nimejaribu kuelezea kwa kifupi au kujibu maswali yako ingawa yako mengi yakuelezea kwa hii topic.Napenda kujua Mother material na mke material yukoje? Je?!! kuna mume material na baba material? lol........

!Grace

2 2gether are always better than he wu is alone

Monday, January 11, 2010

THE WORDS OF A WISE MAN

"The Way You See The Problem Is The Problem"
"Better to write for yourself and have no public, than to write for the public and have no self." Cyril Connolly (1903 - 1974)

MAELEKEZO JINSI YA KUANGALIA PESA HALALI

jana nilikuwa na wadau mahali na nikapata shule jinsi ya kuhakiki uhalali wa noti ya sh.(Tz) 10000/=

1)ULE UPANDE WA TEMBO KWA PEMBENI YAANI KUSHOTO KUNA TARAKIMU 10000. TARAKIMU HIZI UNAWEZA KUZIONA TU UKINYANYUA HIYO NOTI KWA JUU

2) UPANDE WA KULIA MWA PICHA YA TEMBO JUU KIDOGO YA TARAKIMU 10000 KUNA MAANDISHI MADOGO SAAAAAAAAANA AMBAYO NIMESHINDWA KUNG'AMUA NI MAANDISHI YA NINI LAKINI HAKIKISHA YAMEONEKANA.

ANGALIZO

nilipochunguza dondoo hizo hapo juu kwenye zile noti feki sikuweza kuziona. Inaonekana kile 'kiwanda uchwara' hakiwezi kuchomeka hizo chachandu.

siku njema.

Sunday, January 10, 2010

NI NCHI YA WATU WADOGO


Hiyo ni jina la wimbo wa mwanamuziki Erick Wainaina kutoka Kenya aliyotoa kibao hicho akisanifu hali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya nchi ya Kenya.

Siyo Kenya, tu bali sehemu kubwa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, hali ni ile ile. Hapa Tanzania tunaitwa wananchi; na hapo ndipo ninapoanza kutia mashaka ya mwenendo wetu waafrika. 'wananchi' inatokana na neno, 'wana' yaani watoto. Na 'mtoto' sharti apewe mahitaji yake na 'Baba' mpaka afike ule umri wa
kujitegemea.

Kwa bahati mbaya sana, dola za kiafrika kwa manufaa yao binafsi wangependa wataliwa waendelee kuwa wananchi mpaka Yesu atakaporudi. Hii inapelekea uundwaji wa mataifa ya ombaomba na hata ubunifu kidogo alionao mwanadamu unaondolewa kutokana na dhana ya utegemezi unaopaliliwa na viongozi wetu.

Iko wapi Siasa ya ujamaa na kujitegemea? Ingawa wengi watahoji na kujiuliza kwani siasa ya ujamaa na kujitegemea mbona ilidumu kwa miongo takribani mitatu na hatukuendelea? Ninachoweza kujibu ni kwamba aghalabu siasa hiyo iliweka msingi wa kuendelea na ilikuwa ni kazi ya dola kujenga nyumba imara. Abraham Lincoln aliyekuwa Rais wa Marekani aliwahi kuwauliza wamerekani. 'Jiulize utaifanyia nini Marekani, na siyo Marekani itakufanyia nini'. Enzi ya Mwalimu watanzania tulipelekwa katika mwelekeo wa kujitegemea zaidi ya kutegemea. Mtoto wa shule ya msingi bila ya kuwa na tabaka lolote alitegemewa kwenda shule na ufagio wa chelewa kwa wale tuliosoma mjini na kwenda na jembe kwa wale waliosoma vijijini. Shule ya sekondari ilimjenga mwanafunzi kuwajibika mashambani na hata pale alipomaliza kidato cha sita tulitegemewa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa. Hii yote ilikuwa ni katika hali ya kujenga misingi ya kujiamini na kuamsha chachu za kukomaa, ubunifu na kudumisha mapenzi kwa nchi. Mtanzania alijengwa na kuandaliwa kuwa mkulima au mfanyakazi na siyo ombaomba.

OMBA OMBA sasa inaanaanza kuwa ni sehemu ya maisha, yaani ustaarabu wetu, jambo linalonikera kweli kweli. Hata ubunifu na uvumilivu kidogo kama binadamu unatushinda. Hainiingii akilini pale ambapo mtu ananijia na mali mathalani nguo inayochuuzwa na ndugu yake na kuniomba ninunue eti ili nimuunge mkono huyo ndugu yake. Wenyewe tunasema 'muungishe' ndugu yangu. Sasa najiuliza, je nanunua shati kwa sababu ninalihitaji ( need) au kwa sababu ili nikusaidie kuyamudu maisha ya mjini? Hainingii akilini pale ninapoegesha gari langu likiwa safi kabisa na anatoka kijana akiwa na ndoo ya maji akiomba alioshe gari na mwisho wake nimpatie pesa. Ninamwambia kuwa liache hili gari langu ni safi, huyo kijana mwenye nguvu zake za kuendeleza sera ya kilimo kwanza mashambani ananijibu, basi naomba nilioshe unisaidie maji ya kunywa, yaani pesa kidogo. Sasa kijana huyu anauza huduma yake ya kuosha gari au anaomba msaada wa pesa? Heshima ya mtanzania inashuka sana pale mfanyakazi mwenzako ambaye kwa bahati mbaya sana ana mshahara mdogo kukupita wewe anapokuomba, 'Bosi nifanyie 500/= sijala ndugu yako'. Nani atakataa nikisema kuwa nitakapompatia hiyo 500/= ninamdumaza na kudumuza 'utoto wake, i.e mwananchi. Na miye ninayetoa hiyo pesa ninakuwa 'mwenyenchi'.

JE TUTAFIKA?

Saturday, January 9, 2010

MABADILIKO YA HALI YA HEWA


Joto! joto! joto! Tanzania ndani ya nyumba hakukaliki, joto ni kali kweli kweli. Wenzetu walioko Uingereza na Marekani wanasema hata kazini hawaendi kwani theruji imekubali kweli kweli.
Leo Dar Es Salaam temperature ni 32 degrees wakati New York ni -8 degrees.

NOTI FEKI DAR ES SALAAM, TANZANIA


Noti mbili za Tanzanian shillings 10000/=
Hiyo ya kushoto ni feki, ina msitari katikati na inaonyesha kupauka pauka. Nawahatadharisha ndugu na wadau tuwe waangalifu tunapochukua pesa.
Mdogo wangu alichukua 1000,000/= kutoka 'Western Union' na baadaye akakuta 70000/= ni feki.
Ni pale alipoenda kutumia pesa takribani sh. 90000/= ndipo mchuuzi alipomrudishia 40000/= ni kumuelewesha kuwa hizo ni feki. Alipochunguza kale kamilioni kake akagundua 70000/= kati ya hizo ni feki.
Swali kwenu wadau, mbona hizi pesa zilipitishwa kwenye machine? Hiyo machine kazi ya ni nini? mie nilidhani ni kutambua pesa feki.

Friday, January 8, 2010

sauti kutoka kwa kapera

"unatakiwa mwaka 2010 uowe you are grown up"
hii ni kauli ambayo nimeipata humuhumu siku ya leo.Na si leo tu bali kila siku ambayo ndio imenisukuma kuandika hiki ninachokiandika.Naomba kuuliza maswali yafuatayo:
1.Umri gani unafaa kwa mwanaume kuoa na umri wa mwisho mwanaume kuoa ni miaka mingapi?
2.Unaoa ili nini?
3.Unamuoa nani?
4.No regrets/hakuna majuto?
5.Unafuraha?
Ndugu zangu kuoa si kwenda kusafisha nyota ili na wewe uonekane mjini umeoa,mimi naliheshimu sana tukio la ndoa maana ni muunganiko kati ya mwanamke na mwanaume na kuwa kitu kimoja mpaka kifo kitakapowatenganisha kama imani ya dini yangu isemavyo.Mume na mke kufikiri na kutenda kama team moja,kufurahishana,kukasirishana,shida na raha mzipitie pamoja n.k....kuishi na mwenzako miaka nenda rudi ndani ya nyumba moja,chumba kimoja,kitanda kimoja si mchezo kila siku, kuanzisha familia pamoja namengine mengi.Sihitaji kukurupuka kukufurahisha wewe.
Mimi sipo desparate kutaka kuoa am happy na maisha yangu so far,sihitaji mwanamke ndio aje kukamilisha au kuleta furaha katika maisha yangu,am happy with me.
Si kila mwanamke unaekuwa nae kama mpenzi basi lazima umuoe na kuwa mumeo,kuna wakati unakutana na mwanamke mnapendana kabisa lakini kuna vitu ambavyo vinafanya wewe na yeye msiweze kuoana.Kuna ambao si wife material wala mother material.Mwingine hayupo tayari kuolewa muda wake haujafika, mwingine tabia sio zenyewe kabisa.
Am 45 yrs old wala sijihisi kupungukiwa kitu katika maisha yangu...nitaoa muda utakapofika wa kufanya hivyo na mwanamke ambae mimi mtoto p nimeona ananifaa kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu.Kwasababu nitapenda kuwa mwanamme mwenye furaha japo najua ndoa ina mapito mengi lakini kama nitakuwa nimeoa mwanamke anaenipenda na mimi kumpenda tutayapita pamoja.
SITAOA ILI KUUDANGANYA ULIMWENGU KUWA NA MIMI NIMEOA...No one is in charge of my happiness except me....my head is my government.

Thursday, January 7, 2010

African professionalism, mostly an illusion phenomena

Practically professionalism is sacred; it entails moving extra mile in delivering goods and services. It does not only consist of greedy way of making money, nor does it exist on wearing expensive suits, or driving flush car, or applying exotic perfumes. One is not called a professional simply because of his fluency on foreign language, as some idiots seem to suggest.

A truly professional person think outside the box when delivering goods and services.He/she is a servant not a master. If this person is a teacher, his sole goal is to ensure that students passes exams, if this person is a driver, his ultimate goal is to ensure that passengers reaches their destination safely and comfortably. Likewise politicians too are professionals at their own right. We expect them to lead the way and not cheat the electorates.

In most of African countries ( well africa south of sahara), modern professionalism is alien; only recently imported from western world. A century ago, in Africa, teachers existed but not in a formal way but informal circumustances. By then teachers were referred to as appretinces delivering practical lessons to ever eager students that molded them to value driven adults.

Africa had its own indegenious leaders who were greatly envied by sons and daughters. Naturally these leaders were professional in totality, serving their subjects honestly, diligently and immaculately. Leaders delivered social decisions by consensus not by dictation. Even 'judges' were highly respected and not giving verdict while bending on materialistic considerations. Oh, yes, our ancestors had medicine men who were not delivering their service depending on monetary terms, but purely as a social responsibility.

The emergence of money economy has distorted the all meaning of professionalism. Now especially in Africa, cash determines ones access to basic good and services. A patient can not receive basic medical care without money, rule of law can not be applied without money, at worse even church leaders bend their sacred rules in favourwealthy sons of God. It seems every one is chasing money thus erasing professionalism. A 'daladala' driver as he speeds to take a next passenger passes a red light only to bribe a policeman on the next stop; a nurse ignores a patient with no cash, and a policeman poses on our roads waiting for cash from drivers who may commit shoddy traffic offence. Ironically in Dar Police officers are called 'wazee wa fedha' and no one finds this as an insult to a noble profession.

VERDICT

WE ALL LOOK SILLY!

Monday, January 4, 2010

BURIANI SIMBA WA VITA

KAMBARAGE: Ah! Ngoja nipunge upepo hapa nje, mh! Nani yulee anakuja,kama ninamfahamu! Ah! siamini RASHIDI!

Waoooo!! SIMBA WA VITA!!! jamani vipi za huko!

Hajambo MKAPA?, KIKWETE amekua siku hizi? Eh! vipi chama changu?

RASHIDI; Ah! Niache nipumzike! nina mengi, huko hakuna Chama ni ufisadi TU! Hivi nimeacha skendo, Chama kimekwapua MABILIONI, Duh!! nikaona niishie zangu maanake ni kashfa!! nitakupa STORY zaidi, yaani JULIUS utalia!!!