Saturday, March 26, 2011

jamani tunashindwa nini kwenye chakula tunachokula?

jamani waafrika tumepoteza mwelekeo na kwa kweli tunashindwa kutunza kile mababu zetu walichotuachia.

Aliandika Prof Mazrui, kwamba waafrika wanamebadilika ndani ya miaka 30 kwa kasi kubwa zaidi ya wachina miaka 100 iliypita.

Angalia hili suala la chakula. Hivi ni kweli tumeshindwa kuvienzi na kuvitukuza vyakula vyetu vya asili?? hivi ni kweli ni lazima tunywe soda kila siku? Hivi ni kweli bia ndio kinywaji bora cha kujiburudisha? Je tunaweka mazingira gani mbadala ili kukabiliana na madhara ya matumizi ya vyakula vya kisasa??

Ustaarabu tunaoendekeza hauendani na ustaarabu asili wa kwetu. Mzee wangu alinisimulia jinsi ambavyo wenyeji wa kilimanjaro walivyokuwa na dawa ya kunywa iliyosafisha tumbo kumuandaa mla nyama ya mbuzi kupokea kitoweo hicho. Alinisimulia kuwa baada ya kunywa dawa hiyo, mlaji wa kitoweo cha mbuzi angeweza kula mbuzi kwa wingi sana bila kumletea madhara ya afya.

Sasa tunachoweka mdomoni kinatuumbua kwa kutuletea magonjwa ambayo zamani yalionekana kuwa ni ya wazee. Vijana wadogo wa miaka 20-30 wanapata kisukari, shinikizo la damu,nk kisa wanakula vyakula kama vile nyama nyekundu,wanakunywa bia,wanakunywa soda nyingi( iliyojaa sukari tele). Enzi za mababu zetu, vyakula vililiwa lakini wazee wetu walikuwa wanatembea maili nyingi hivyo waliweza kuunguza mafuta kirahisi.

ebu tuwaangalie hao wazungu tunawaona kama kioo cha maendeleo. Wao wana Diet coke, wana sweeteners(mbadala wa sukari) na wanakunywa maziwa kwa wingi,samaki siyo adimu kama ilivyo Afrika nk.

Matokeo ya chakula kisicho bora ndiyo haya ya kukimbilia kwa Babu!!!!

Mmmh yangu macho.

No comments:

Post a Comment