Saturday, March 26, 2011

KUHUSU AJALI YA WASANII:Mdomo uumba!!!

Ni msemo wa siku nyingi lakini una maana yenye mashiko.

Mdomo uumba. Wiki iliyopita watanzania tulighubikwa na taarifa mbaya ya ajali ambapo wanamuziki wa bendi ya mwondoko wa taarabu walikutwa na mauti pale ambapo dereva mzembe alipowaua.

Maneno ni makali lakini utamuelezeaje dereva aliyekuwa anakwenda mwendo wa kasi kiasi cha kushindwa kuhimili machine ya mzungu? Kilichotokea mzembe yule alilengesha gari kwa dereva mwingine wa lori aliyekuwa mzembe na kuharibikiwa lori bila kuweka ishara ya kuonyesha kuwa gari lake ni bovu. Dereva yule mpumbavu wa wasanii akijaribu kulipita lori bovu lililosimama alipoona lori lingine linamjia uso kwa uso akalipeleka gari lake upande wa lori lililosimama na hivyo kuwaua abiria ( wasanii) waliokaa upande wa kushoto mwa gari.

Kilichonisikitisha na staili ya jinsi hiyo stori ilivyotangazwa na vyombo vyetu vya habari. Hakuna chombo cha habari kilichofanya utafiti wa kina wa uthibitisho kama yule dereva alikuwa na leseni halali ama la? je alikuwa amelewa? je dereva wa lile lori bovu alipotelea wapi? Nani mwenye lile lori bovu? kwanini vyombo vya habari haviku watafuta waliosababisha ajali hiyo na kuwahoji? mbona hakukuwa na 'press conference' yenye maswali ya maana kwa polisi??

jamani mdomo uumba. Kama vyombo vyetu vya habari vitaishia na maneno ya kipumbavu kama vile 'tuwaombee marehemu wameenda kwa kumuumba' tutakufa wengi jamani.

Mdomo wetu ndio unaoumba ajali.

No comments:

Post a Comment