Thursday, April 7, 2011

LEADERS CLUB BONANZA; WATEULE MNATUANGUSHA

Wateule wa kipato cha kati mnakataa historia? Si mlisoma historia jamani!!! wapi matumizi ya historia ya Mkwawa mliyofundishwa na wazee wenu. Au mnawakufuru.

Tunaambiwa kuwa hivi karibuni kutakuwa na Bonanza pale Leaders Club ambapo mashabiki wa timu kali za Ulaya watachuana na kuwaonyeshana 'ubabe' wa kisoka. Ingawa ni muhimu kwa binadamu wa kawaida kufanya mazoezi na kupasha misuri, ninachokataa ni ajenda inayotumika katika kupashana misuri hapo Leaders Club.

Wanaendesha bonanza hili ni kundi la watu tunaowaita 'wateule'( intelligensia) au kwa lugha ya kuazima wanaitwa 'Middle class'. Sasa katika hizi dhama za harakati ya kimapinduzi kama inavyoshuhudiwa Libya, Algeria, Misri na kwingeneko, kwa kweli hatutakiwi kushangaa na kuwa na starehe hii tuliyonayo. Jamani, tuulizane sisi wateule tulio Dar Es Salaam tunashindwa kuungana nguvu zetu na kufanya mabonanza ya kimapinduzi? Tukumbuke hizo timu tunazoshabikia za Barcelona, AC Milan, Manchester, nk zimeundwa baada ya wananchi wa nchi hizi kupigania mapinduzi ya ukweli mpaka wakawa na demokrasia ya ukweli yenye kuwapa utu wananchi wao.

Ikimbukwe 1848 kulikuwepo na mapinduzi ya uhakika Ufaransa, Uhispania na Italia, mapinduzi yaliyoweka mbegu ya hizi timu tunazoshabikia kibudu kibudu. Tunaijua historia ya AC Milan, au tunapiga makelele kwenye luninga kizembe zembe tu?

Kwa kushindwa kuwaangunisha wakulima wa vijijini katika vita ya kuungoa UFISADI ulioshamiri; tunawasaliti watemi wetu akina Mtemi Mkwawa!!!

Tuamke wanasheria, wasomi wa mlimani, wahandisi, na madktari, mapinduzi ya Misri, Libya, yanaletwa na makundi haya. Sie twapiga kelele za Mau U

OLE WETU.

1 comment:

  1. Tuamke wanasheria, wasomi wa mlimani, wahandisi, na madktari, mapinduzi ya Misri, Libya, yanaletwa na makundi haya. Sie twapiga kelele za Mau U. ni uamsho mzuri lakini mbona unaamsha wasomi tu wakati majority ya umma ni tofauti na hawa?

    ReplyDelete