Saturday, April 16, 2011

UMUHIMU WA HESABU

ulishawahi kufikiria na kujiuliza umuhimu wa namba katika maisha yako ya kila siku.
1) Asubuhi unaamshwa na 'alarm' ya saa iliyoandikwa namba

2) unaangalia saa yako na kuizima na kuendelea kulala
Baada ya muda alarm hiyo hiyo iliondikwa namba inakusumbua tena

3) Unaamka na kabla ya kuondoka unabonyesha microwave iliyo 'display' namba na kupasha moto weetabix

4) halafu unavaa viatu viliondikwa namba 9

5) Halafu unaingia na kuwasha gari yenye 'speedometer' zilizoandikwa namba

6) Unasafiri na baadaye unafika nje ya ofisi yako na kusogelea kibox kinaitwa 'teller machine' kilichoandikwa namba

7) Kimashine hicho kinatoa noti ambazo zimeandikwa namba na unazihesabu kwa kutumia namba

8) Unaingia ofisini na bosi wako anaangalia kidude mkononi mwake chenye kuonyesha namba, tunakiita saa na anakupigia kelele kuwa umechelewa.

9) Kisha unapokea 'handover' kutoka kwa mwenzako kwenye karatasi iliyosheenezwa namba, wenyewe mnaita takwimu.


10) Unagundua simu yako ya mkononi aina salio na unamuita tarishi unampatia noti iliyoandikwa namba aende nje akakuchukulie 'voucher'. Anakuletea voucher na kisha unakwangua na kukuta namba. Unaziingiza hizo namba kwenye simu yako na kuruka hewani.

List haitaisha ni mwendelezo mrefu sana.

Hii yaonyesha kuwa toka enzi hizo namba zimetawala Dunia.

Husimnyime haki yake mwanao kwa kutomfundisha hesabu.Wanaojua kuchanganya changanya hizo namba na kutoa logic ndio wanaondesha ulimwengu.

Tafakari, Chukua hatua, Haki Elimu.

No comments:

Post a Comment