Thursday, February 25, 2010

MBONA HATUTUMII RASLIMALI ZETU?

Dola nyingi za kiafrika zinawaangalia wapiga kura wake kwa jicho la dharau, kutowajali na kufanya kazi kwa mazoea bila kujua kuwa wao ndiyo 'engine' ya maendeleo. Matokeo yake dola hizi zinashawishika mara kwa mara kukimbilia nchi za nje kuomba misaada.

Siye wananchi kwa makundi yetu twaweza, wala hatuhitaji $$$ kuendesha maisha yetu.Tunapozongwa na matatizo mengi twatafuta njia mbadala ya kutatua matatizo yetu na twaiweka kando serikali kuu, twazipiga kisogo serikali za mitaa, na kujihimu wenyewe.

Sasa hii ina maana gani? wakati dola inapokosa kuwajibika kwa wapiga kura wake, kinachotokea ni kwamba wapiga kura nao hawaoni umuhimu wa kuwajibika kwa dola. Wengi hatulipi kodi, na wala hatuoni umuhimu wa kufanya hivyo. Lakini kodi tunayolipa ni kwa njia tofauti na labda hatuoni kuwa ni kodi halali. Tunapotoa michango ya harusi hiyo ni kodi ya aina yake kwani tunategemea huyo tunayemchangia naye atusaidie wakati wa shida; tunapotembelea wagonjwa hospitali tunawekeza kwa ajili ya matatizo ya usoni; tunapohudhuria misiba hatupotezi muda ila ni amana tunayorudishiwa pale na siye majanga yatakapotugusa. Waingereza wanasema, 'scratch my back and I will scratch yours'.

Wala hatuhitaji kwenda nchi za magharibi kuomba misaada!!!!! Baba wa Taifa aliwahi kusema hivi, ' Ili tuendelee twahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watu tunao wengi tu na kwa kweli uwiano wa wanaozaliwa huku juu kuliko wanaokufa; ardhi tunayakutosha, ila kinachokosekana ni siasa safi na uongozi bora wa kutumia vizuri raslimali watu na ardhi nchi iliyojawaliwa na Mwenyezi Mungu. Majuzi tulishuhudia janga la mafuriko kule kilosa, Morogoro. Nguvu tulizonazo kama watanzania zilijidhihirisha pale ambapo Radio binafsi na Kampuni ya simu vilivyoendesha kwa ufanisi mkubwa zoezi la kuchangisha pesa zilizowasaidia waanga wa yale mafuriko. Hii yaonyesha nguvu za ndani ya nchi zinavyoweza kufanya maajabu.

Serikali hamuoni nguvu za wananchi????????

No comments:

Post a Comment