Kinachojiri hapa Dar Es Salaam ni stori ambazo mie ninayeishi katika nguvu za mwanga 'enlightment' ninapata taabu sana kuziamini. Lakini kwa kuwa jamii inayonizunguka inazipigia upatu napaswa niendane na jamii hii.
jana kwa majibu ya radio clouds ( dar es salaam fm station) ni kwamba pale katika daraja maarufu la salender kumeonekana mambo ya ajabu. Mtoa taarifa ameshindwa kusema tukio hili lilitokea lini jambo ambalo linazidi kutuchanganya wanajamii. Eti mwanamke mmoja alikuwa kwenye gari akisubiria foleni kwenye mataa. Akatokea ombaomba akiomba msaada. Mwanamama huyo akashusha kioo na kutoa msaada wa pesa. Alaaaaah! ghafla mkono wake ukaanza kutoa manyoya ya paka na huku ukawa unavimba. Mwanamke huyo akamuuliza yule ombaomba nimekukosea nini? mbona mkono wangu unabadilika? Yule ombaomba hakujibu. Kwa kuwa traffic warden alisharuhusu magari na yule mama akawa anachelewesha foleni alichokifanya yule warden ni kumfuata yule mama na kumuuliza kulikoni?? mbona haundeshi gari? Yule mama akamuonyesha mkono ulivyovimba na kumueleza umeanza kuvimba na kubadilika alipotoa msaaada wa pesa. Traffic warden akamuuliza ombaomba imekuwaje??? Ombaomba akasema mkono utapona pale ambapo mwanamke yule atambusu. Toba!!! mwanamke akatoka ndani ya gari na kumbusu yule ombaomba. Alipombusu tu, wote wakayeyuka!!!!!!!!!!! salala.
Tena, siku tatu zilizopita, Radio Clouds ikatupa nyingine kali; katika kipindi chake cha jioni maarufu kama JAHAZI, kikiendeshwa na watangazaji wawili mahiri, Gadner Jihabeshi na Efrahim Kibonde wakisoma magazeti ya jioni walisoma habari moja kutoka gazeti la Dar Leo nalo likitoa mauzauza. Eti, mfanyakazi wa ndani ( Maid) alikutwa na mwajiri wake usiku wa manane akiwa uchi wa mnyama chumbani kwake huku amekalia ndoo na kuongea lugha hisiolewekwa. ( Alikuwa anawanga).Mwajiri ikabidi aiamshe familia nzima na walipomdadisi akakiri kuwa bibi yake huwa anatembelea familia hiyo usiku akitokea Tanga na huwa anatumia ungo na kuja kuwachezea familia nzima( Haikuelezwa anawachezea kivipi!!!). Mdada huyo vile vile akakiri kuwa alishawahi kuua mtoto mmoja huko alipokuwa anafanya kazi kabla hajaja kwenye familia hiyo. Zaidi Baba mwenye nyumba alikiri kuwa huwa anajisikia uchovu kila aamkapo asubuhi. jamani jamii ya kitanzania inakwenda wapi??
Siyo zamani sana takribani miaka 100 iliyopita, waafrika tulivamiwa na wazungu ( hasa wamissionari) ambao kwa sababu walizozijua wao wakauita ustaarabu ( culture) wetu kuwa ni wa kishenzi na kishetani. Tulilazimishwa kuachana na ustaarabu wetu na kukumbatia ustaarabu wa kizungu. Dini ya kigeni ( kikristu na kiislamu), muundo wa kiuchumi, lugha ya kigeni ( ingawa watanzania tunapigana sana kukienzi kiswahili) nk nk. Miaka 100 baadaye bado mababu wanalia huko waliko. Bado hizo ambazo siye wa kileo tunaziita nguvu za giza zinaonyesha na kupiga kelele ya ukunga ' NA SIYE TUPO'.
Mwanazuoni Ali Mazrui katika kazi yake 'The Africans' ( Page, 11) anaandika na ninamnukuu
The ancestors of Africa are angry. For those who believe in the power of the ancestors, the proof of their anger is all around us. For those who do not believe in ancestors, the proof of their anger is given another name. In the words of Edmund Burke, 'People will not look forward to posterity who never look back to their ancestors. But what is the proof of the curse of the ancestors? Things are not working in Africa. From Dakar to Dar Es Salaam, from Marrakesh to Maputo, institutions are decaying, structures are rusting away. It is as if the ancestors had pronounced the curse of cultural sabotage.
Cha ajabu serikali yetu ya Tanzania yadai kwamba haiamini uchawi!!! ingawa wananchi wake na hata viongozi wake wanashabikia uchawi na ushirikina. Kwanini wanashabikia?? jibu ni kwamba uchawi na ushirikina ni sehemu ya mapokeo yetu, ni ustaarabu wetu. Hatuwezi kuachana nao. Tulishuhuudia mwaka jana ambapo watunga sheria wetu tena ndani ya BUNGE letu tukufu walipowekeana upupu( powder ambazo mkemia mkuu alishindwa kutambua ni nini) kwenye viti!!!!!!!!! mmhhhh
Kama serikali inakaa kimya na kutofuatilia kwa karibu ustaarabu wa wananchi wake, sehemu nyingine yenye nguvu sana na yenye ushawishi mkubwa kwa jamii haikai kimya. HII NI DINI. Miezi kadhaa iliyopita maaskofu wa kikatoliki walikutana Vatican na katika 'resolution' yao waliamua kwamba kila askofu achague padre atakayekuwa 'mtaalam' wa kushughulikia uchawi na ushirikina. Wakotoliki wanajua wazi kwamba ili waweze kuwa 'on top of the game' ni lazima wawashughulikie wachawi kwani wenzao walokole wanatoa mapepo; karama ambayo inawapatia waumini wengi.
Ajabu ni kwamba viongozi wetu mmoja mmoja wanatabia ya kwenda kuaguliwa lakini hawako tayari kuuweka uchawi na ushirikina katika sera na mipango ya kitaifa. Viongozi wetu wanataka kuunda sera na mipango yenye 'support' na pesa ya misaada kutoka kwa wafadhiri tabia ambao inaonyesha ni ubinafsi uliotukuka na ukosefu wa ubunifu.
TUSIDANGANYANE WATANZANIA
WENGI TUNAAMINI UCHAWI NA USHIRIKINA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ina maaana huyo MWANAMKE hakuonekana tena?!!!
ReplyDeleteNa je wewe unaamini nini? mie sihamini hizo ndoto za abnuasi! Untill when I can witness with my naked eyes, then work out te scenarios behind such scene.
ReplyDelete