Wednesday, June 8, 2011

HUWEZI KUONA MSITU UNAPOKUA MSITUNI; UTAONA MITI TU

Ni lini ulikunywa maji kutoka bombani, (kutoka bomba la dawasco), ni lini ulikunywa maziwa? Ni lini uliumwa na kuitiwa gari la wagonjwa (ambulance)? Ni lini ulilala hapa jijini Dar Es Salaam bila kutumia chandarua? Ni lini ulipanda daladala na kukuta hakuna mtu aliyesimama?

Maswali ni mengi, mengi sana; na inapofika mahala tunapokuwa kwenye lindi la dhiki na shida na tukaona kawaida, au tunapopotezea, tunajizidishia ujinga ndani ya vichwa vyetu.Kizazi hiki cha nyoka, hiki kizazi kilichozaliwa miaka 80 na 90 ni kizazi kilichojikuta kwenye msitu na huku hakijui kuwa kipo kwenye msitu. Anayegundua kuwa kijana huyu yupo msituni ni yule aliyeishi miaka ya 60 na 70 ambapo enzi hizo hatukuwa na misitu.

Ni sisi wenye miaka 40 na kuendelea tuliyeonja maji ya bombani, ni sisi tulisoma shule za msingi za serikali na leo tunafanya kazi kwa umakini maofisini. Ni sisi ambao hatukuishi na matenki ya maji darini, ambapo sasa inaonekana kuwa ndiyo ustaarabu. Ni sisi ambao Baba zetu walifaidi barabara za lami kwa kuendesha 'bito'( vokswageni) na kuyapitisha yale magari madogo kwenye lami zilisheheni jijini Dar-Es-Salaam. Ni sisi tuliyefaidi treni ya reli ya kati kutoka Dar kwenda mikoani.

Leo hii kijana anayeanza kazi, hana upeo wa kumuuliza diwani wake, barabara ya lami iko wapi? yeye anachowaza ni kutafuna rushwa na kununua prado.

Tafakari, chukua hatua.

No comments:

Post a Comment