Nachopenda kuhusu waganga wa kienyeji ni kwamba wanatumia uoto wa asili kama vile wanasayansi wa magharibi wanavyotegemea mimea hiyo hiyo katika kutengeneza dawa. Tulichokosea sisi waafrika ni kwamba mara baada ya kuja kwa wageni miaka 500 iliyopita tulipumbazwa na kusahau ustaarabu wetu wa kuwa karibu na ardhi na mimea yetu. Leo hii waafrika tunategemea tafiti za kizungu katika kutatua matatizo ya kimatibabu. Ingekuwa vyema tungekubali kurudi enzi za zama na kuwafadhiri akina Dr. Manyuki na wao wapige hatua za kitibabu. Tukubali kuwa kuendelea kutegemea dawa za kigeni na muundo mzima wa kimatibabu wa kimagharibu kunatugharimu sana na hatutafika mbali kimaendeleo. Leo hii Tanzania inatumia 10% ya bajeti yake katika nyanja ya kitabibu lakini wagonjwa na magonjwa mengi yanaibuka hata yale yaliyokuwa hayapo miaka 100. Huko vijijini huduma za kitibabu ni nadra kupatikana na huko ndiko akina Dr Manyuki wanapata heshima na wateja wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment