Thursday, January 28, 2010

MFUMO UMEMUUA SWETU FUNDIKIRA

Wiki hii vyombo vya habari vya Tanzania vimegubikwa na taarifa ya mauaji ya kusikitisha ambapo kijana mmoja aitwaye Swetu Fundikira alipigwa na hatimaye kupata majeraha yaliyomsababishia kifo mara pale alipokimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam. Taarifa zinafafanua kwamba wanajeshi watatu waliokuwa wanatoka katika kumbi ya starehe walighazibishwa baada ya gari lao kuchunwa na gari la Sweti. Kilichofuata ni kipigo cha uhakika.

Vifo kama hivi vimekuwa ni kawaida sana ingawa misiba mingine inakuwa siyo rahisi kumngamua muuaji kutokana na mazoea ya mfumo wetu tuliozoea. Kwa waafrika 'kifo' ni suala nyeti sana ( sacred) na jamii yetu haitoi nafasi ya kuzungumzia chanzo cha kifo. Kwa kuwa kifo ni majariwa ya mwenyezi Mungu na wala hatuna upeo wa kuzungumzia ni nini chanzo cha kifo fulani, basi tunakaribisha vifo vingine kirahisi sana. Hata kama tutatoa lawama kwa wale wanajeshi, je tunajua umakini wa wahudumu na waganga wa pale Muhimbili katika zile harakati za kuyaokoa maisha ya marehemu? Je, Marehemu Swetu alitolewa pale eneo la tukio na usafiri wa aina gani? Sijafuatialia hili lakini nina wasiwasi kama gari lililokamilika la wagonjwa ( fully equipped ambulance) lilitumika katika kumsafirisha kuelekea Muhimbili. Tuwarudie wale maaskari; Nikisema kwamba hawakuwa na 'reference point' ya adhabu nyingine kali iliyotolewa na wauaji/ watesaji kama wao nitakuwa nimekosea?

Siku tatu kabla ya kifo cha Swetu, rafiki yangu alipata ajali ya pikipiki ambapo alilivaa 'truck' barabara ya morogoro majira ya saa mbili za jioni. Rafiki yangu hakuwa na 'helmet' na inasadikika kuwa alikuwa amekunywa pombe. Barabara ya moro kipande kile haina taa za barabarani, na wala lile lori halikuwa limewasha taa. Haya ndiyo mazingira yaliyomuua rafiki yangu, ni mfumo mzima na wala siyo majariwa ya mwenyezi Mungu. Nilipohudhuria msiba wa rafiki yangu, hakuna hata mtu mmoja kati ya watu waliopewa nafasi ya kutoa hotuba pale mazikoni aliyewaasa watu hasa vijana kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa. Pale msibani walikuwepo viongozi wa serikali za mitaa, lakini tulishindwa kuwaambia kuhusu umuhimu wa taa za barabarani. Waingereza wanasema, 'we should take the bull by its horns'.

Mwezi huu nilizika mke wa rafiki yangu ya mpenzi, kilichomuua? operesheni ya uzazi!!!!, cha kushangaza pamoja na majonzi makubwa tuliokuwa nayo, hatukuwa na muda wa kufuatilia kwa kina 'ni nini hasa kilichojiri kwenye chumba cha upasuaji'. Kufanya hivi siyo kumtafuta mchawi ila ni katika jitihada ya kujua chanzo kamili ili kuzuia misiba mingine ya ndugu zetu wapendwa.

Lakini kwa waafrika, hata ninapoandika hili naogopa kuonekana nakufuru kwani 'kifo' hakizungumziwi; KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA. We should call a spade a spade. Nakumbuka Nelson Mandela alipokuwa anamzika mtoto wake alisema wazi wazi, kuwa mwanae amekufa kwa ukimwi. Ila huku kwetu marehemu hasemwi vibaya.

TUNAJIUA WENYEWE NA KWA UHAKIKA TWAZIDI KUFA.

2 comments:

  1. Haloo Kaka,
    Habari za mida?
    Ni masikitiko makubwa juu ya kifo cha bwana Swetu na pia naikubali hoja yako hapo juu. Hata hivyo sijui wapi pa kuanzia, lakini mimi nadhani kama ulivyosema, kila sehemu inahusika kwa aina moja au nyingine katika kuchangia matendo haya ambayo kabisa yanaweza kuepukika bila hata ya gharama ya aina yoyote ile. Pia naweza sema elimu ama busara ya kuzaliwa nayo pia inakosekana. Kweli hao wahusika (wanajeshi)wangekuwa wao ndo wameikwangua gari ya Swetu, wangekubali kupigwa na kuuawa? Je, kulikuwa na uhakika gani kwamba pengine wao ndo hawakuzingatia sheria za barabarani mpaka wakapelekea gari yao kukwanguliwa? Pengine masikini pande zote si kosa lao, bali ni barabara mbovu, bila alama (traffic warning signs), etc? vyovyote vile au katika hali yoyote iliyokuwepo pale wakati wa tukio, hakukuwa na sababu ya kuchukua sheria mkononi. Uhai wa mwanadamu yeyote yule hapa duniani bado unayo thamani kubwa kuliko vfifaa(objects/materials) vingine. Kwahiyo, kama ulivyosema, mfumo wetu mzima ndiyo unasababisha masuala mengine kama haya.....
    (ntaendelea baadae kidogo)

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa tunamalizwa na mfumo. Isitoshe serikali iliyopo madarakani inajali maslahi kuliko utu. Ingekuwa ni mkubwa kigogo amepigwa au kupata ajali ingefuatiliwa na kuundwa kamati na taa kuwekwa kesho yake, au mtu kuchukuliwa hatua lakini raia wa kawaida mmhhh!!!! Kama alikuwa amelewa kwa nini traffic hawakumzuia barabarani ili kuokoa maisha yake? Kazi yao ni nini? na hiyo helmet hawakuona kama hajavaa wamzuie? Kuhusu huyo mzazi watu huchukulia bahati mbaya, mapenzi ya Mungu. na hata hao madaktari hawapati mshikemshike wa kufuatiliwa ndo maana itatokea tena kwa mwingine kwa sababu imekuwa kawaida kwetu kusema bahati mbaya. Hatuweki mambo wazi ukiwa muwazi unatengwa na kuchukiwa na wasiopenda haki , kwa hiyo watu wengi wanapenda kuonekana wazuri na hali tunajimaliza wenyewe. N juu yetu sasa kubadilika na kuwa huru na serikali yetu ili kubadilisha mfumo huu.

    ReplyDelete