Saturday, October 24, 2009

Fatiki ya Rwanda

Chanzo cha BBC swahili service kinatutaarifu kuwa nchini Rwanda, serikali ya Mjeshi Kagame imeamua kufanya tathmini kwa wafanyakazi wake wa serikali kila mwezi, ambapo alama kama zile za shule zitakuwa zinatolewa kwa watumishi wa Umma.

Chanzo hicho kinatutaarifu kuwa mtumishi wa umma atakayepata alama kati ya 70-100% ataendelea na kazi na ikiwezekana atapandishwa cheo. Alama 50-69% atasimamishwa kazi na kupewa nafasi ya kutuma maombi ya ajira upya, ambapo yule atakayepata chini ya alama 50% anafukuzwa kazi.

Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumishi wa umma kuwa wale viongozi wa vitengo vya serikali ambao ndio wanaotoa hizo alama wanaweza kuwa na visasi na waajiriwa hivyo kutoa maamuzi ya upendeleo, ( Victimization).

Wewe hii unaionaje?

Watumishi wa serikali ya Tanzania wamekuwa na tabia ya uzembe, ubadhirifu, ulaji wa rushwa na kwa ujumla kuwajibika kumekuwa kwa mashaka sana. Nakumbuka miaka ya 1990's Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliwahi kutangaza upitishwaji wa Fagio la chuma kwa watumishi wazembe. Vile vile miaka hiyo hiyo aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, mpiganaji Augustino Lyatunga Mrema alianzisha tabia ya kuvamia ofisi za serikali na kuondosha viti vya mtendaji aliyekuwa hayupo kazini.

Licha ya juhudi hizi za zima moto? bado watumishi wa serikali wamekuwa wakifanya kazi kimazoea, kusuasua na kivivu.

Tanzania, tufanye nini?

No comments:

Post a Comment