Tuesday, October 6, 2009

JANA ILIKUWA SIKU YA MAKAZI DUNIANI

Jana 5th of October ilikuwa ni siku ya makazi duniani; lakini pale eneo la kimara nje ya jiji la Dar es salaam kanisa katoliki lina ugomvi wa kiwanja na shangazi yangu. Kihistoria kanisa lina jadi ya kupanuka, hulka hii ilikuwepo tangu enzi ya Mt. Paulo alieneza injili siyo tu Jerusalem bali pia nje ya mitaa yake na kuelekea Cypress, Pamphylia, Pisidia, and Lycaonia, na sehemu kubwa ya Asia. Vile vile alieneza injili Pisidian Antioch, Iconium, Lystra, and Derbe. Kanisa linataka kumpatia 34m/= takribani $28,000, pesa ambayo hawezi kupata nyumba yenye dhamani ya nyumba yake. Mmh hili ni jina la Bwana hama la shetani?

Shangazi ana hati mkononi, lakini kanisa bado halijatuonyesha hiyo hati yao wanaodai wanayo.

No comments:

Post a Comment