Thursday, October 15, 2009

NI WIKI YA KUJISOMEA

Nani kasema watanzania hatupendi kusoma? hapa ni asubuhi maeneo ya Mwenge kituoni. Kama walivyo mabosi, mtanzania wa kawaida anapenda kujua nini kinaendelea katika nchi yake. Survey hii nilivyoifanya mchana nilikuta 'newstands' zikiwa hazina watu wanaopiga 'chabo' kama ilivyo asubuhi. Pale mwenge nilizubaa kwa muda hiyo asubuhi na niliweza kushuhudia wapitia njia wakisoma gazeti bila kununua. Wazungu walisema, 'do not read a book by its cover'. Viongozi wetu wanaposiliana na wananchi kupitia vyombo vya habari hususani magazeti ujumbe wao hauwafikii walengwa kwa muda husika na hali hii inafanya wananchi wasiweze kujua kinachoendelea ndani ya nchi yao wenyewe.

Sababu kubwa inayofanya 'wadanganyika' kushindwa kusoma 'morning news' ni ukosefu wa kipato kwani kwa wastani bei ya gazeti ni 500/= wakati wananchi wengi tunaishi chini ya $1 kwa siku.

Ila kuna njia mbadala ya kuhakikisha kuwa siye wananchi tunapata habari kila siku na hivyo kujua viongozi wetu wanatuambia nini au wanafanya nini. Kwanini tusiwaige wazungu mambo ya maana badala ya kuiga vitu vya kipuuzi. Mfano nchini Uingereza halmashauri za miji zinachapisha na kusambaza magazeti kwa wakazi wa miji bure huku makampuni ya miji hiyo yakigharimia magazeti hayo kwa kutangaza matangazo. Kwa kufanya hivyo wananchi wanapata habari ya kinachoendelea katika miji yao na wakati huo huo halmashauri za miji zinapata faida na kuwa na pesa za kuendesha miji.

Tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wanatarijiwa kupiga kura huku wakiwa 'mbumbumbu' bila kujua mipango ya viongozi wao. Ama kweli wajinga ndio waliwao.

No comments:

Post a Comment