Monday, September 28, 2009

ardhi inalipa


Hapa kagondo, nanasi nne (4) ni shillingi 1000/=. Kama Tanzania ingeweza kuboresha miundombinu na kuwezesha hizi nanasi kufika mijini kwa urahisi wote tungefaidi. Wakulima kijijini na walaji mjini. Lakini kwa mwendo huu wa masaa 30 ya kufika kijijini kutokea dar es salaam, mkulima hatazidi kudodewa na hayo matunda yake yasiyo na dhamani. Na siye mjini tutazidi kuona matunda ni anasa. Labda siku moja kutakuwa na viwanda vya kusindika matunda pale Bukoba mjini na kupunguza ile msukumo wa vijana kukimbilia Dar Es Salaam kuganga njaa. labda viwanda vikiwa vingi pale Bukoba Mjini kutaleta hamasa ya vijana kujishughulisha na kilimo cha matunda kijijini badala kungangania ndizi na kahawa.

No comments:

Post a Comment