Lakini kama Msomi Ali Mazrui alivyowahi kusema, 'The only thing we as africans need to change is our own changebility'; muda wote tunabadilisha mazingira yetu yaendane na mazingira ya wanaotutawala.
Leo Dar inangara kwa prado, Vx, hammer, na magari kibao ya Fwd kutoka japan, wakati hao hao wageni waliotupa baiskeli ndio wanaotupa magari. Bado barabara zetu hazikutengenezwa kwa ajili ya waendesha baiskeri. Barabara hasa za Dar ni nyembamba kuruhusu magari na baiskeri kupita kwa wakati mmoja. Na hata pale mjasiri anapoamua kuendesha baiskeri, ana hatarisha maisha yake kwa vile madereva wetu wanatumia njia hizo hizo zinazotegemewa kutumia waendesha baiskeri.
No comments:
Post a Comment