Saturday, September 12, 2009

ULINZI NA USALAMA WA DAR ES SALAAM NI UOZO MTUPU!!

Nimekuwa nikiishi nchini Uingereza kwa takribani miaka tisa! ni miaka mingi ukizingatia kuwa niliondoka mwaka 1999 nikiwa na miaka 29. Maisha yamebadilika sana katika nyanja zote! Mojawapo ya sekta ya umma inayonipa mashaka makubwa na kuhatarisha usalama wangu hapa nyumbani ni chombo cha polisi!

Ndio Uingereza inaitwa nchi ya dunia ya kwanza, lakini hili siyo kisingizio kwa kwa nchi yangu Tanzania kuwa na secta ya usalama hisiwajibika kwa wananchi wake.

Utawala wa sheria ni mpangilio wa utaratibu ambapo matukio yanayotokea kila siku yanaendana na sheria. Tunapokuwa hatuna sheria kila mtu atafanya anachotaka kufanya na hapo ndipo mnyonge anapodondoshwa na mwenye nguvu. Kiujumla serikali haiwezi kuwa kamilifu kama hakuna utawala wa sheria.

Ninaishi Dar Es Salaam, mji mkuu wa Tanzania wenye wakazi takribani millioni 4, na wilaya tatu za kiutawala, i.e Temeke, Ilala, na Kinondoni. Dar Es Salaaam kama ilivyo miji mingine duniani inapaswa kutawalaliwa na utawala wa sheria.

Majuzi jirani alivamiwa na vibaka wakati alipokuwa anaelekea kazini. Cha ajabu ni kwamba ukiwa barabarani utakutana na idadi kubwa ya askari wa usalama wa barabarani wakipunga magari yapite. Idadi hii haina uwiano na idadi iliyopo kwenye vitongoji vyetu.

Kibaya zaidi, hali imekuwa tete kiasi kwamba mwananchi wa kawaida hana elimu ya uraia inayomuelimisha kutambua kuwa polisi anawajibu kwake. Leo hii nikivamiwa na majambazi nikiwa natembea mtaani siwezi kutupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kusimamia amani na usalama wangu. Tunapofika kwamba mwananchi wa kawaida anakosa imani na polisi basi ni vigumu kwa mwananchi huyo huyo kuwa na imani na serikali iliyopo madarakani. Kwani Polisi ni chombo muhimu sana cha dola.

Matukio tunayoyaona kwa wananchi kujichukulia madaraka mikononi na kuwachoma moto watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi ni hatari kwa usalama wa Taifa. Sifahamu ni lini nitachomwa moto. Au kirahisi kirahisi mtu niliyemzidi akili kwa kitu fulani chochote tu, anaweza kutuma wahuni wakapiga kelele mwiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii huyoooooooooooo! na nikachomwa moto kirahisi sana.

Juzi lilitokea tukio ambalo lilinisikitisha sana. Rafiki yangu ninayefanya naye kazi aligundua kuwa mke wake ananyemelewa na rafiki yake kipenzi. Kilichoendelea ni kuwa huyo rafiki yangu alipanga na mke wake waweke mtego kwamba huyo mke wake akubali kutoka na rafiki yake waende nyumba ya wageni ( Geust House). Rafiki huyo alichukua mapolisi wawili wakavamia hiyo nyumba ya wageni na kumpiga huyo mgoni wake na kumjeruhi vibaya sana. Mgoni huyo aliugulia siku tatu majeraha ya kupigwa na polisi. Je huo ulikuwa ni utawala wa sheria? Is this not the assault case? Hii ni nchi ya wastaarabu? Kibaya zaidi pale kazini hakuna mtu aliyekuwa na busara na kuona tatizo katika ule uamuzi wa polisi waliopewa dhamana ya kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na sheria na utaratibu. Maswali ya hekima inabidi yaulizwe.
Je, ni uvunjaji wa sheria kwenda nyumba ya wageni na mwanamke zaidi ya miaka 18?
Ni sheria ipi inayompa madaraka polisi kumpiga raia kwenye nyumba ya wageni?
Je, siyo ukweli kuwa kesi hiyo ingepelekwa mahakamani yule mgoni angeshinda?

Kuna tatizo kubwa la weredi ( Professionalism) hapa Tanzania. Jeshi la Polisi lina tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wenye upeo mdogo wa mawazo watasema kwamba tatizo hili linatokana na kipato kidogo wanachopewa polisi wetu. Tatizo siyo kipato, kama mtu anaona kazi fulani haina maslahi kwanini hasiiache hiyo kazini na kufanya kazi nyingine?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

1 comment:

  1. Amnbacho wangefanya polisi ni kuwachukua na kuwapeleka vyombo vya sheria, lakini kwa sababu wanapenda "kitu kidogo" hawakufanya hivyo. Kwanini huyo mgoni hakwenda kwenye vyombo vya sheria? (kushtaki) au ndio wanavyosemaga aibu? na kwanini hiyo G.house waruhusu swala la hatari kama hilo? Mwisho wake ingekuwa kifo then marehemu anabambikiziwa kesi ya wizi au kushindana na polisi.... We call.. Sheria mkononi.

    ReplyDelete