Monday, September 28, 2009

KWENDA KWETU, MSAFIRI NI ZAIDI YA KAFIRI

Baada ya safari ya karibu masaa 30, nilifika kijijini kwetu kwa kupanda pikipiki iliyonipitisha na kunipandisha mabonde na milima. Lazima niseme kwamba naogopa sana kupanda chombo cha moto kinachoendeshwa bila kufuata minimum standards kama kuvaa helmet. Hapa Kagera pikipiki ni usafiri rasmi wa kuelekea migombani kusikopitisha magari. Sidhani kama dereva wangu alikuwa na leseni. Mmmh lakini nilifika salama. Hapa nyumbani maisha ni kudra ya Mwenyezi Mungu.

No comments:

Post a Comment