Tuesday, September 29, 2009

kanisa katoliki kabarenge

Big up to Fr Deusdedit Byabato, mtu mzima huyu alizaliwa na kusoma na kukulia kijijini kabarenge. Sasa anaeneza injili Illinois, USA. Mtu kwao bwana amerudisha fadhira kwa ku facilitate ujenzi wa kanisa la kisasa hapa kijijini. Dini imekubali bwana.

Miaka 17 iliyopita nilipokuwa naishi kijijini hapa, tulikuwa tunasali katika kanisa la miti na matope lilisokafiwa majani. Ingependeza kama wadau wengine waishio ughaibuni wangependelea nyumbani kwao kama Fr Deus. Tunao Madaktari, wahandisi, manesi, na kada nyingine nyingi tu walioko pembe zote za duniani. Wherever we go, home is the best!

No comments:

Post a Comment